مَا كَانَ لِأَهْلِ ٱلْمَدِينَةِ وَمَنْ حَوْلَهُم مِّنَ ٱلْأَعْرَابِ أَن يَتَخَلَّفُوا۟ عَن رَّسُولِ ٱللَّهِ وَلَا يَرْغَبُوا۟ بِأَنفُسِهِمْ عَن نَّفْسِهِۦ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ لَا يُصِيبُهُمْ ظَمَأٌ وَلَا نَصَبٌ وَلَا مَخْمَصَةٌ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا يَطَـُٔونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ ٱلْكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِۦ عَمَلٌ صَٰلِحٌ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ ٱلْمُحْسِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHaiwafailii watu wa Madina na Mabedui walio kando kando yao kusalia nyuma wasitoke pamoja na Mtume, wala kujipendelea nafsi zao kuliko nafsi yake. Hayo ni kwa sababu wao hakiwapati kiu, wala machovu, wala njaa, katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaendi mahali panapowaghadhibisha makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, isipokuwa huandikiwa kwa hicho kitendo chema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanaofanya uzuri.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHaiwafalii watu wa Madina na Mabedui walio jirani zao kubakia nyuma wasitoke na Mtume, wala kujipendelea nafsi zao kuliko yeye. Hayo ni kwa kuwa hakiwapati kiu, wala machofu, wala njaa, kwa ajili ya Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawendi mahali panapo waghadhibisha makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, ila huandikiwa kuwa ni kitendo chema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanao fanya mema.