فَرِحَ ٱلْمُخَلَّفُونَ بِمَقْعَدِهِمْ خِلَٰفَ رَسُولِ ٱللَّهِ وَكَرِهُوٓا۟ أَن يُجَٰهِدُوا۟ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَقَالُوا۟ لَا تَنفِرُوا۟ فِى ٱلْحَرِّ قُلْ نَارُ جَهَنَّمَ أَشَدُّ حَرًّا لَّوْ كَانُوا۟ يَفْقَهُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalifurahi walioachwa nyuma kwa kule kukaa kwao nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na wakachukia kupigana Jihadi kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wakasema: Msitoke kwenda katika joto! Sema: Moto wa Jahannamu una joto kubwa zaidi, laiti wangelikuwa wanafahamu!
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWalifurahi walio achwa nyuma kwa kule kubakia kwao nyuma na kumuacha Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walichukia kupigana Jihadi kwa mali zao na nafsi zao, na wakasema: Msitoke nje katika joto! Sema: Moto wa Jahannamu una joto zaidi, laiti wangeli fahamu!