caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura At-Tawba, Aya 16

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 113 · 9:16

أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تُتْرَكُوا۟ وَلَمَّا يَعْلَمِ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ جَٰهَدُوا۟ مِنكُمْ وَلَمْ يَتَّخِذُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَا رَسُولِهِۦ وَلَا ٱلْمُؤْمِنِينَ وَلِيجَةً وَٱللَّهُ خَبِيرٌۢ بِمَا تَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, mlidhani kuwa mtaachwa tu, na Mwenyezi Mungu hajawajua wale waliopigana Jihadi miongoni mwenu, na wala hawakumfanya yeyote mwendani wao isipokuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini wenziwe? Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniJe, mlidhani kuwa mtaachwa tu, bila ya Mwenyezi Mungu kuwajuulisha wale walio pigana Jihadi kati yenu, na wala hawakumfanya mwendani wao isipo kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini wenziwe? Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70