وَأَذَٰنٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦٓ إِلَى ٱلنَّاسِ يَوْمَ ٱلْحَجِّ ٱلْأَكْبَرِ أَنَّ ٱللَّهَ بَرِىٓءٌ مِّنَ ٱلْمُشْرِكِينَ وَرَسُولُهُۥ فَإِن تُبْتُمْ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ وَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِى ٱللَّهِ وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni tangazo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwaendea watu wote siku ya Hija Kubwa kwamba Mwenyezi Mungu yuko mbali na washirikina, na Mtume wake pia yuko mbali. Kwa hivyo, mkitubu, basi hilo ndilo heri kwenu. Na mkigeuka, basi jueni kuwa nyinyi hamuwezi kumshinda Mwenyezi Mungu. Na wabashirie wale waliokufuru adhabu chungu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa ni tangazo kutokana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wote siku ya Hija Kubwa kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawana jukumu lolote kwa washirikina. Basi mkitubu itakuwa kheri kwenu, na mkigeuka basi jueni kuwa nyinyi hamumshindi Mwenyezi Mungu. Na wabashirie makafiri kuwa watapata adhabu chungu.