caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura At-Tawba, Aya 69

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 113 · 9:69

كَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ كَانُوٓا۟ أَشَدَّ مِنكُمْ قُوَّةً وَأَكْثَرَ أَمْوَٰلًا وَأَوْلَٰدًا فَٱسْتَمْتَعُوا۟ بِخَلَٰقِهِمْ فَٱسْتَمْتَعْتُم بِخَلَٰقِكُمْ كَمَا ٱسْتَمْتَعَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُم بِخَلَٰقِهِمْ وَخُضْتُمْ كَٱلَّذِى خَاضُوٓا۟ أُو۟لَٰٓئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَٰلُهُمْ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ وَأُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَٰسِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi kama wale waliokuwa kabla yenu. Walikuwa wana nguvu na mali na watoto zaidi kuwaliko nyinyi. Basi walistareheka kwa fungu lao, na nyinyi mnastareheka kwa fungu lenu, kama walivyostareheka kwa fungu lao wale waliokuwa kabla yenu. Na nyinyi mkazama katika maovu kama wao walivyozama. Hao, matendo yao yaliharibika katika dunia na Akhera; na hao ndio waliohasiri.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNi kama wale walio kuwa kabla yenu. Walikuwa wana nguvu na mali na watoto zaidi kuliko nyinyi. Basi walistarehea fungu lao, na nyinyi mnastarehea fungu lenu, kama walivyo starehe kwa fungu lao wale walio kuwa kabla yenu. Na nyinyi mkazama katika maovu kama wao walivyo zama. Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika katika dunia na Akhera; na hao ndio walio khasiri.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70