caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura At-Tawba, Aya 117

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 113 · 9:117

لَّقَد تَّابَ ٱللَّهُ عَلَى ٱلنَّبِىِّ وَٱلْمُهَٰجِرِينَ وَٱلْأَنصَارِ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ فِى سَاعَةِ ٱلْعُسْرَةِ مِنۢ بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ إِنَّهُۥ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu alikwishakubali toba ya Nabii na Wahajiri na Ansari waliomfuata katika saa ya ugumu, baada ya kwamba nyoyo za kundi miongoni mwao zilikuwa zimekaribia kukengeuka. Basi akakubali toba yao. Hakika Yeye kwao ni Mpole, Mwenye kurehemu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu amekwisha pokea toba ya Nabii na Wahajiri na Ansari walio mfuata katika saa ya dhiki, pale baada ya kukaribia nyoyo za baadhi yao kugeuka. Basi akapokea toba yao, kwani hakika Yeye kwao wao ni Mpole na ni Mwenye kuwarehemu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70