أَمْ حَسِبَ ٱلَّذِينَ ٱجْتَرَحُوا۟ ٱلسَّيِّـَٔاتِ أَن نَّجْعَلَهُمْ كَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ سَوَآءً مَّحْيَاهُمْ وَمَمَاتُهُمْ سَآءَ مَا يَحْكُمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, wanadhani wale wanaotenda maovu kuwa tutawafanya wawe sawasawa na wale walioamini, na wakatenda mema, uhai wao na kufa kwao? Ni hukumu mbaya mno wanayoihukumu!
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniJe! Wanadhani wanao tenda maovu kuwa tutawafanya kama walio amini, na wakatenda mema, sawa sawa uhai wao na kufa kwao? Ni hukumu mbaya wanayo ihukumu!