أَفَرَءَيْتَ مَنِ ٱتَّخَذَ إِلَٰهَهُۥ هَوَىٰهُ وَأَضَلَّهُ ٱللَّهُ عَلَىٰ عِلْمٍ وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمْعِهِۦ وَقَلْبِهِۦ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِۦ غِشَٰوَةً فَمَن يَهْدِيهِ مِنۢ بَعْدِ ٱللَّهِ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, umemwona aliyefanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akampoteza pamoja na kuwa ana elimu, na akaziba masikio yake, na moyo wake, na akambandika kifuniko kwenye kuona kwake? Basi ni nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Je, hamkumbuki?
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniJe! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki?