Swahili Translation - Rowad Translation CenterHatukuziumba mbingu na ardhi wala yaliyo baina yake ila kwa haki na kwa muda maalumu. Na wale waliokufuru wanayapuuza yale wanayoonywa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Je, mwawaona wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu? Nionyesheni wameumba nini katika ardhi; au hao wanalo fungu katika mbingu zote? Nileteeni Kitabu kilichokuwa kabla ya hiki, au alama yoyote ya elimu, ikiwa mnasema kweli.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni nani mpotovu mkubwa kuliko hao wanaoomba badala ya Mwenyezi Mungu wale ambao hawatawaitikia mpaka Siku ya Kiyama, na wala hata hawatambui maombi yao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale waliokufuru husema juu ya haki inapowajia: 'Huu ni uchawi dhahiri.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu wanasema: 'Ameizua mwenyewe!' Sema: 'Ikiwa nimeizua mimi, basi nyinyi hamwezi kunifaa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Yeye anajua zaidi hayo mnayoropokwa; anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi. Na Yeye ndiye Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: 'Mimi si kitu kigeni miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyofanywa mimi wala nyinyi. Mimi nafuata niliyofunuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji wa wazi wazi.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: 'Mnaonaje yakiwa haya ni kweli yametoka kwa Mwenyezi Mungu, nanyi mmeyakufuru, na akashuhudia shahidi miongoni mwa Wana wa Israili juu ya mfano wa haya, na akaamini, na nyinyi mnafanya kiburi? Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliokufuru waliwaambia wale walioamini: 'Lau kuwa hii ni heri, wasingelitutangulia kuifikia.' Na walipokosa kuongoka, wakasema: 'Huu ni uzushi mkubwa wa zamani.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kabla yake kilikuwapo Kitabu cha Musa, chenye uongozi na rehema. Na hiki ni Kitabu cha kusadikisha na kilichokuja kwa lugha ya Kiarabu, ili kiwaonye wale waliodhulumu, na kiwe ni bishara njema kwa watendao mema.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tumemuusia mwanadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu, na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thelathini. Hata anapofika utu uzima wake, na akafikilia miaka arubaini, husema: 'Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayoyapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ndio tunaowapokelea bora ya vitendo vyao walivyovitenda, na tunayasamehe makosa yao. Watakuwa miongoni mwa watu wa Bustani za mbinguni. Miadi ya kweli hiyo waliyokuwa wakiahidiwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa yule aliyewafyonya wazazi wake: 'Uff kwenu nyote. Ati ndio mnanitisha kuwa nitafufuliwa, na hali vizazi vingi vimekwisha pita kabla yangu!' Na hao wazazi humwomba msaada Mwenyezi Mungu (na humwambia mtoto wao): 'Ole wako! Amini! Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli.' Na yeye husema: 'Hayakuwa haya ila ni visa vya watu wa kale.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ndio ambao imehakikishwa hukumu juu yao kama mataifa yaliyokwisha pita kabla yao miongoni mwa majini na watu. Hakika hao wamekuwa wenye kuhasiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wote watakuwa na daraja zao mbalimbali kwa waliyoyatenda, na ili awalipe kwa ukamilifu kwa vitendo vyao, na wala hawatadhulumiwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku watakapoletwa wale waliokufuru kwenye Moto, wataambiwa: 'Nyinyi mlitwaa vitu vyenu vizuri katika uhai wa duniani, na mkajistarehesha navyo. Basi leo ndio mnalipwa adhabu ya fedheha kwa yale mlivyokuwa mkitakabari katika ardhi bila ya haki, na kwa sababu mlikuwa mkivuka mipaka.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mtaje ndugu wa kina 'Adi, alipowaonya watu wake kwenye vilima vya mchanga. Na kwa yakini waonyaji wengi walitokea kabla yake na baada yake kuwaambia: 'Msimuabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu. Hakika mimi nawahofia ije kukupateni adhabu ya siku iliyo kuu.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: 'Je, umetujia ili ututenge mbali na miungu yetu? Basi tuletee hayo unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: 'Hakika ujua wa hayo uko kwa Mwenyezi Mungu. Mimi nawafikishieni yale niliyotumwa nayo. Lakini nawaona kuwa nyinyi mnafanya ujinga tu.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi walipoliona wingu likielekea kwenye mabonde yao, walisema: 'Hili ni wingu la kutunyeshea mvua!' Kumbe sivyo, haya ni hayo mliyotaka yawajie haraka: upepo ambao ndani yake imo adhabu chungu!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterUnaharibu kila kitu kwa amri ya Mola wake Mlezi. Wakawa hawaonekani ila nyumba zao tu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo watu wahalifu!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka tuliwaweka vizuri siyo kama tulivyokuwekeni nyinyi, na tuliwapa uwezo wa kusikia, na kuona na ufahamu wa nyoyo. Na hayakuwafaa uwezo wao wa kusikia, na kuona na ufahamu wa nyoyo kwa lolote. Kwani hao walikuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara ndiyo yakawafika.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mbona wale waliowashika badala ya Mwenyezi Mungu, kuwa ati hao ndio wawakurubishe, hawakuwanusuru? Bali waliwapotea! Na huo ndio uongo mkubwa waliokuwa wakiuzua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakati tulipowaleta kundi la majini kuja kwako kusikiliza Qur-ani. Basi walipoihudhuria, walisema: 'Sikilizeni!' Na ilipokwisha somwa, walirudi kwa kaumu yao kwenda kuwaonya.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: 'Enyi kaumu yetu! Hakika sisi tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya Musa, kinachosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake, na kinachoongoza kwenye Haki na kwenye njia iliyonyooka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi kaumu yetu! Muitikieni Mwenye kuitia kwa Mwenyezi Mungu, na muaminini, Mwenyezi Mungu atawasamehe, na atawakinga kutokana na adhabu chungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wasiomwitikia Mwitaji wa Mwenyezi Mungu, basi hao hawatashinda katika ardhi, wala hawatakuwa na walinzi mbele yake. Hao wamo katika upotovu ulio dhahiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawaoni ya kwamba Mwenyezi Mungu, aliyeziumba mbingu na ardhi, na hakuchoka kwa kuziumba, kuwa ni Muweza wa kuwafufua wafu? Kwani? Hakika Yeye ni Muweza mno wa kila kitu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku watakapoletwa makafiri Motoni, wakaambiwa: 'Je, haya si kweli?' Watasema: 'Ndivyo? Tunaapa kwa Mola wetu Mlezi, ni kweli!' Atasema: 'Basi onjeni adhabu kwa sababu ya vile mlivyokuwa mkikufuru.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi subiri, kama walivyosubiri Mitume wenye stahmala kubwa, wala usiwafanyie haraka. Siku watakayoyaona hayo waliyoahidiwa, itakuwa kama kwamba hawakukaa ulimwenguni ila saa moja ya mchana. Huu ndio ufikisho! Kwani huangamizwa wengine isipokuwa watu wavukao mipaka tu?