caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Ash-Shams الشمس

Aya 15 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 26

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ وَٱلشَّمْسِ وَضُحَىٰهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNinaapa kwa jua na mwangaza wake!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلْقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa mwezi unapolifuatia!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa mchana unapolidhihirisha!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa usiku unapolifunika!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa mbingu na kwa aliyeijenga!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلْأَرْضِ وَمَا طَحَىٰهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa ardhi na kwa aliyeitandaza!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّىٰهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa nafsi na kwa aliyeitengeneza!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَىٰهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha akaifahamisha uovu wake na wema wake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّىٰهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika amefanikiwa aliyeitakasa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّىٰهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika amehasiri aliyeiviza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَىٰهَآ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotovu wao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشْقَىٰهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAliposimama mwovu wao mkubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقْيَٰهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipowaambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمْ فَسَوَّىٰهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا يَخَافُ عُقْبَٰهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala Yeye haogopi matokeo yake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70