caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-A'laa الأعلى

Aya 19 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 8

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ سَبِّحِ ٱسْمَ رَبِّكَ ٱلْأَعْلَى

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLitakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِى خَلَقَ فَسَوَّىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAliyeumba, na akaweka sawa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِى قَدَّرَ فَهَدَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ambaye amekadiria na akaongoa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِىٓ أَخْرَجَ ٱلْمَرْعَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa aliyeotesha malisho.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحْوَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha akayafanya makavu, meusi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTutakusomesha wala hutasahau.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُ إِنَّهُۥ يَعْلَمُ ٱلْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIla akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhahiri na yaliyofichikana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tutakusahilishia yawe mepesi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكْرَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi kumbusha, kama makumbusho yanafaa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAtakumbuka mwenye kuogopa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَتَجَنَّبُهَا ٱلْأَشْقَى

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa atajitenga mbali nayo mpotovu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِى يَصْلَى ٱلنَّارَ ٱلْكُبْرَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbaye atauingia Moto mkubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTena humo hatakufa wala hawi hai.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika amekwisha fanikiwa aliyejitakasa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَذَكَرَ ٱسْمَ رَبِّهِۦ فَصَلَّىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بَلْ تُؤْثِرُونَ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini nyinyi mnapendelea maisha ya dunia!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلْـَٔاخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ هَٰذَا لَفِى ٱلصُّحُفِ ٱلْأُولَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

صُحُفِ إِبْرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterVitabu vya Ibrahimu na Musa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70