caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Muhammad محمد

Aya 38 · Madina · mpangilio wa kuteremshwa 95

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَصَدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ أَضَلَّ أَعْمَٰلَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, Yeye atavipotoa vitendo vyao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَءَامَنُوا۟ بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٍ وَهُوَ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ كَفَّرَ عَنْهُمْ سَيِّـَٔاتِهِمْ وَأَصْلَحَ بَالَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale walioamini, na wakatenda mema, na wakaamini yale aliyoteremshiwa Muhammad - nayo ni Haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi - atawafutia makosa yao na ataitengeneza hali yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱتَّبَعُوا۟ ٱلْبَٰطِلَ وَأَنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱتَّبَعُوا۟ ٱلْحَقَّ مِن رَّبِّهِمْ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ أَمْثَٰلَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa sababu wale waliokufuru wamefuata upotovu, na wale walioamini wamefuata Haki iliyotoka kwa Mola wao Mlezi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowapigia watu mifano yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِذَا لَقِيتُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فَضَرْبَ ٱلرِّقَابِ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَثْخَنتُمُوهُمْ فَشُدُّوا۟ ٱلْوَثَاقَ فَإِمَّا مَنًّۢا بَعْدُ وَإِمَّا فِدَآءً حَتَّىٰ تَضَعَ ٱلْحَرْبُ أَوْزَارَهَا ذَٰلِكَ وَلَوْ يَشَآءُ ٱللَّهُ لَٱنتَصَرَ مِنْهُمْ وَلَٰكِن لِّيَبْلُوَا۟ بَعْضَكُم بِبَعْضٍ وَٱلَّذِينَ قُتِلُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَلَن يُضِلَّ أَعْمَٰلَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mnapowakuta wale waliokufuru, wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha, wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe. Ndivyo hivyo. Na lau angelitaka Mwenyezi Mungu, angeliwashinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu awatie mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na wale waliouliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu, hatayapoteza matendo yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَيَهْدِيهِمْ وَيُصْلِحُ بَالَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAtawaongoza na awatengezee hali yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيُدْخِلُهُمُ ٱلْجَنَّةَ عَرَّفَهَا لَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa atawaingiza katika Pepo aliyowajuulisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تَنصُرُوا۟ ٱللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu, naye atakunusuruni na ataiimarisha miguu yenu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فَتَعْسًا لَّهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَٰلَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliokufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا۟ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَٰلَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa sababu waliyachukia yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَلَمْ يَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ دَمَّرَ ٱللَّهُ عَلَيْهِمْ وَلِلْكَٰفِرِينَ أَمْثَٰلُهَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani hawakutembea katika ardhi wakaona ulikuwaje mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Mwenyezi Mungu aliwaangamiza, na kwa makafiri hawa itakuwa mifano ya hayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ مَوْلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَأَنَّ ٱلْكَٰفِرِينَ لَا مَوْلَىٰ لَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa wale walioamini. Na makafiri hawana mlinzi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱللَّهَ يُدْخِلُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ جَنَّٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَٰرُ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يَتَمَتَّعُونَ وَيَأْكُلُونَ كَمَا تَأْكُلُ ٱلْأَنْعَٰمُ وَٱلنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mwenyezi Mungu atawaingiza wale walioamini na wakatenda mema katika Bustani za mbinguni zipitiwazo na mito kati yake. Na wale waliokufuru hujifurahisha na hula kama walavyo wanyama, na Moto ndio makazi yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ هِىَ أَشَدُّ قُوَّةً مِّن قَرْيَتِكَ ٱلَّتِىٓ أَخْرَجَتْكَ أَهْلَكْنَٰهُمْ فَلَا نَاصِرَ لَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni miji mingapi iliyokuwa na nguvu zaidi kuliko mji wako huu uliokutoa? Tuliwateketeza na wala hawakuwa na yeyote wa kuwanusuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّهِۦ كَمَن زُيِّنَ لَهُۥ سُوٓءُ عَمَلِهِۦ وَٱتَّبَعُوٓا۟ أَهْوَآءَهُم

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, yule aliye kwenye ubainifu kutoka kwa Mola wake Mlezi ni kama yule aliyepambiwa uovu wa vitendo vyake, na wakafuata matamanio yao?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَّثَلُ ٱلْجَنَّةِ ٱلَّتِى وُعِدَ ٱلْمُتَّقُونَ فِيهَآ أَنْهَٰرٌ مِّن مَّآءٍ غَيْرِ ءَاسِنٍ وَأَنْهَٰرٌ مِّن لَّبَنٍ لَّمْ يَتَغَيَّرْ طَعْمُهُۥ وَأَنْهَٰرٌ مِّنْ خَمْرٍ لَّذَّةٍ لِّلشَّٰرِبِينَ وَأَنْهَٰرٌ مِّنْ عَسَلٍ مُّصَفًّى وَلَهُمْ فِيهَا مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ وَمَغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ كَمَنْ هُوَ خَٰلِدٌ فِى ٱلنَّارِ وَسُقُوا۟ مَآءً حَمِيمًا فَقَطَّعَ أَمْعَآءَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMfano wa Bustani ya mbinguni waliyoahidiwa wacha Mungu, ina mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa yasiyoharibika ladha yake, na mito ya mvinyo wenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyosafishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakaodumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayochemka ya kuwakatakata matumbo yao?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ حَتَّىٰٓ إِذَا خَرَجُوا۟ مِنْ عِندِكَ قَالُوا۟ لِلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ مَاذَا قَالَ ءَانِفًا أُو۟لَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَٱتَّبَعُوٓا۟ أَهْوَآءَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wapo miongoni mwao wanaokusikiliza, mpaka wakiondoka kwako, huwauliza waliopewa elimu: 'Amesema nini sasa hivi?' Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu ameziba nyoyo zao, na wakafuata matamanio yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ ٱهْتَدَوْا۟ زَادَهُمْ هُدًى وَءَاتَىٰهُمْ تَقْوَىٰهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale walioongoka anawazidishia uongofu na anawapa ucha Mungu wao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا ٱلسَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً فَقَدْ جَآءَ أَشْرَاطُهَا فَأَنَّىٰ لَهُمْ إِذَا جَآءَتْهُمْ ذِكْرَىٰهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani wanangojea jengine isipokuwa iwafikie Saa (ya Kiyama) kwa ghafla? Na hakika alama zake zimekwisha kuja. Na itakapowajia, kutawafaa nini kukumbuka kwao?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱعْلَمْ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ وَٱسْتَغْفِرْ لِذَنۢبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَٰتِ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ وَمَثْوَىٰكُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi, na mahali penu pa kukaa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَوْلَا نُزِّلَتْ سُورَةٌ فَإِذَآ أُنزِلَتْ سُورَةٌ مُّحْكَمَةٌ وَذُكِرَ فِيهَا ٱلْقِتَالُ رَأَيْتَ ٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ نَظَرَ ٱلْمَغْشِىِّ عَلَيْهِ مِنَ ٱلْمَوْتِ فَأَوْلَىٰ لَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Waumini wanasema: 'Kwa nini haiteremshwi Sura?' Na inapoteremshwa Sura madhubuti na ikatajwa ndani yake habari ya vita, utawaona wenye maradhi katika nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anayezimia kwa sababu ya mauti. Basi ni bora kwao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

طَاعَةٌ وَقَوْلٌ مَّعْرُوفٌ فَإِذَا عَزَمَ ٱلْأَمْرُ فَلَوْ صَدَقُوا۟ ٱللَّهَ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterUtiifu na kauli njema. Na jambo likishaazimiwa, basi wakiwa ni wakweli kwa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka itakuwa ni heri kwao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوٓا۟ أَرْحَامَكُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mnatarajia kwamba mkigeuka mkaenda zenu kwamba ndio mtafanya uharibifu katika nchi na muwatupe jamaa zenu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أُو۟لَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَعَنَهُمُ ٱللَّهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَىٰٓ أَبْصَٰرَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ndio aliowalaani Mwenyezi Mungu, na akawatia uziwi, na akawapofua macho yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ ٱلْقُرْءَانَ أَمْ عَلَىٰ قُلُوبٍ أَقْفَالُهَآ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawaizingatii hii Qur-ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli zake?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ ٱرْتَدُّوا۟ عَلَىٰٓ أَدْبَٰرِهِم مِّنۢ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلْهُدَى ٱلشَّيْطَٰنُ سَوَّلَ لَهُمْ وَأَمْلَىٰ لَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika wale wanaorudi nyuma baada ya uongofu kwisha wabainikia, Shetani huyo amewashawishi na amewaghuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا۟ لِلَّذِينَ كَرِهُوا۟ مَا نَزَّلَ ٱللَّهُ سَنُطِيعُكُمْ فِى بَعْضِ ٱلْأَمْرِ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ إِسْرَارَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa sababu waliwaambia wale waliochukia yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu: 'Tutakutiini katika baadhi ya mambo.' Na Mwenyezi Mungu anajua siri zao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكَيْفَ إِذَا تَوَفَّتْهُمُ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَٰرَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi itakuwaje Malaika watakapowafisha wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo yao!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ ٱتَّبَعُوا۟ مَآ أَسْخَطَ ٱللَّهَ وَكَرِهُوا۟ رِضْوَٰنَهُۥ فَأَحْبَطَ أَعْمَٰلَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa sababu wao waliyafuata yale yaliyomchukiza Mwenyezi Mungu na wakachukia yanayomridhisha, basi akaviangusha vitendo vyao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ حَسِبَ ٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَن لَّن يُخْرِجَ ٱللَّهُ أَضْغَٰنَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, wenye maradhi nyoyoni mwao wanadhani kwamba Mwenyezi Mungu hatazidhihirisha chuki zao?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْ نَشَآءُ لَأَرَيْنَٰكَهُمْ فَلَعَرَفْتَهُم بِسِيمَٰهُمْ وَلَتَعْرِفَنَّهُمْ فِى لَحْنِ ٱلْقَوْلِ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ أَعْمَٰلَكُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tungelipenda, tungelikuonyesha hao na ungeliwatambua kwa alama zao. Lakini bila ya shaka utawajua kwa namna ya msemo wao. Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ حَتَّىٰ نَعْلَمَ ٱلْمُجَٰهِدِينَ مِنكُمْ وَٱلصَّٰبِرِينَ وَنَبْلُوَا۟ أَخْبَارَكُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka tutawajaribu mpaka tuwajue wapiganao Jihadi katika nyinyi na wanaosubiri. Nasi tutazifanyia mtihani habari zenu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَصَدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَشَآقُّوا۟ ٱلرَّسُولَ مِنۢ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلْهُدَىٰ لَن يَضُرُّوا۟ ٱللَّهَ شَيْـًٔا وَسَيُحْبِطُ أَعْمَٰلَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu na wakapingana na Mtume baada ya uongofu kwisha wabainikia, hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote. Naye ataviangusha vitendo vyao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُوا۟ ٱلرَّسُولَ وَلَا تُبْطِلُوٓا۟ أَعْمَٰلَكُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume, wala msiviharibu vitendo vyenu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَصَدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ثُمَّ مَاتُوا۟ وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يَغْفِرَ ٱللَّهُ لَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, kisha wakafa na hali ni makafiri, Mwenyezi Mungu hatawasamehe makosa yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَا تَهِنُوا۟ وَتَدْعُوٓا۟ إِلَى ٱلسَّلْمِ وَأَنتُمُ ٱلْأَعْلَوْنَ وَٱللَّهُ مَعَكُمْ وَلَن يَتِرَكُمْ أَعْمَٰلَكُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi msilegee na mkataka suluhu, maana nyinyi ndio mtakaoshinda. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatawanyima malipo ya vitendo vyenu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّمَا ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَإِن تُؤْمِنُوا۟ وَتَتَّقُوا۟ يُؤْتِكُمْ أُجُورَكُمْ وَلَا يَسْـَٔلْكُمْ أَمْوَٰلَكُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika uhai wa duniani ni mchezo na pumbao. Na mkiamini na mkamcha Mungu, Mwenyezi Mungu atakupeni ujira wenu, wala hatakutakeni mali zenu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِن يَسْـَٔلْكُمُوهَا فَيُحْفِكُمْ تَبْخَلُوا۟ وَيُخْرِجْ أَضْغَٰنَكُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akikutakeni hizo na kukushikilieni, mtafanya ubahili, na atatoa undani wa chuki zenu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَٰٓأَنتُمْ هَٰٓؤُلَآءِ تُدْعَوْنَ لِتُنفِقُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَمِنكُم مَّن يَبْخَلُ وَمَن يَبْخَلْ فَإِنَّمَا يَبْخَلُ عَن نَّفْسِهِۦ وَٱللَّهُ ٱلْغَنِىُّ وَأَنتُمُ ٱلْفُقَرَآءُ وَإِن تَتَوَلَّوْا۟ يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوٓا۟ أَمْثَٰلَكُم

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAngalieni! Nyinyi hawa mnaitwa mtumie mali katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wapo katika nyinyi wanaofanya ubahili. Na anayefanya ubahili, basi anajifanyia ubahili mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka, atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70