Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yajayo, na akutimizie neema zake, na akuongoe katika njia iliyonyooka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili wazidi Imani juu ya Imani yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye elimu mno, Mwenye hekima.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli awaingize Waumini wanaume na Waumini wanawake katika Bustani za mbinguni zipitazo mito chini yake, wadumu humo, na awafutie makosa yao. Na huko ndiko kufuzu kukubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa awape adhabu wanafiki wanaume na wanafiki wanawake, na washirikina wanaume na washirikina wanawake, wanaomdhania Mwenyezi Mungu dhana mbaya. Utawafikia mgeuko mbaya, na Mwenyezi Mungu awakasirikie, na awalaani, na awaandalie Jahanamu. Na hayo ni marudio maovu kabisa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mumsaidie, na mumheshimu, na mumtakase (Mwenyezi Mungu) asubuhi na jioni.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBila ya shaka wale wanaokupa kiapo cha utii, kwa hakika wanampa Mwenyezi Mungu kiapo cha utii. Mkono wa Mwenyezi Mungu uko juu ya mikono yao. Kwa hivyo, avunjaye ahadi hizi, basi anavunja kwa kuidhuru nafsi yake. Na anayetekeleza aliyomuahadi Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu atamlipa ujira mkubwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatakuambia mabedui waliobaki nyuma: 'Zimetushughulisha mali zetu na ahali zetu, basi tuombee msamaha.' Wanasema kwa ndimi zao yasiyokuwamo katika nyoyo zao. Sema: 'Ni nani awezaye kukusaidieni chochote kwa Mwenyezi Mungu akitaka Yeye kuwadhuru au akitaka kuwanufaisha? Bali Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini mlidhani kwamba Mtume na Waumini hawatarudi kabisa kwa ahali zao, na mkapambiwa hayo katika nyoyo zenu, na mkadhania dhana mbaya, na mkawa watu wanaoangamia.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu ndiye mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Humsamehe amtakaye, na humuadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwingi wa kurehemu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaambie wale walioachwa nyuma katika mabedui: 'Mtakuja itwa kwenda kupigana na watu wakali kwa vita, mpigane nao au wasalimu amri. Basi mkimtii, Mwenyezi Mungu atawapa ujira mzuri. Na mkigeuka kama mlivyogeuka kwanza, atawaadhibu kwa adhabu iliyo chungu.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKipofu hana lawama, wala kiguru hana lawama, wala mgonjwa hana lawama. Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, atamuingiza katika Mabustani ya mbinguni yapitayo mito chini yake. Na atakayegeuka upande, atamuadhibu kwa adhabu chungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika Mwenyezi Mungu amewaridhia Waumini walipokuwa wanakupa ahadi ya utii chini ya mti, na alijua yaliyomo nyoyoni mwao. Basi akateremsha utulivu juu yao, na akawalipa kwa Ushindi wa karibu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu anawaahidi ngawira nyingi mtakazozichukua, basi amewatangulizia hizi kwanza, na akaizuia mikono ya watu isiwafikie, na ili hayo yawe ni Ishara kwa Waumini, na akawaongoza njia iliyonyooka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa yale mengine hamwezi kuyapata bado, Mwenyezi Mungu amekwisha yazingira. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza mno wa kila kitu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu uliokwisha pita zamani, wala hutapata mabadiliko katika mwendo wa Mwenyezi Mungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Yeye ndiye aliyeizuia mikono yao kwenu, na mikono yenu kwao, katika bonde la Makka baada ya kuwapeni Ushindi juu yao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mno myatendayo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ndio waliokufuru na wakawazuia msiingie Msikiti Mtakatifu, na wakawazuilia dhabihu kufika mahala pao. Na lau si wanaume Waumini na wanawake Waumini msiowajua mkawasaga na mkaingia makosani kutokana nao bila ya kujua... Mwenyezi Mungu (amefanya haya) ili amuingize amtakaye katika rehema yake. Lau wangelitengana, bila ya shaka tungeliwaadhibu wale waliokufuru kwa adhabu chungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterPale wale waliokufuru walipotia katika nyoyo zao hasira, hasira za kijinga, Mwenyezi Mungu aliteremsha utulivu juu ya Mtume wake na juu ya Waumini, na akawalazimisha neno la kumcha Mungu. Na wao walikuwa ndio wenye haki nalo na wenye kustahili. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua mno kila kitu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mwenyezi Mungu amemtimizia Mtume wake ndoto ya haki. Bila ya shaka nyinyi mtauingia Msikiti Mtakatifu, Inshallah (Mwenyezi Mungu akipenda), kwa amani, na hali mmenyoa vichwa vyenu na mmepunguza nywele. Hamtakuwa na hofu. Yeye anajua msiyoyajua. Basi atawapea kabla ya haya Ushindi karibuni.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki, ili aipe ushindi juu ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMuhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na wale walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kutokana na athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa.