caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Ahqaf, Aya 26

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 66 · 46:26

وَلَقَدْ مَكَّنَّٰهُمْ فِيمَآ إِن مَّكَّنَّٰكُمْ فِيهِ وَجَعَلْنَا لَهُمْ سَمْعًا وَأَبْصَٰرًا وَأَفْـِٔدَةً فَمَآ أَغْنَىٰ عَنْهُمْ سَمْعُهُمْ وَلَآ أَبْصَٰرُهُمْ وَلَآ أَفْـِٔدَتُهُم مِّن شَىْءٍ إِذْ كَانُوا۟ يَجْحَدُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka tuliwaweka vizuri siyo kama tulivyokuwekeni nyinyi, na tuliwapa uwezo wa kusikia, na kuona na ufahamu wa nyoyo. Na hayakuwafaa uwezo wao wa kusikia, na kuona na ufahamu wa nyoyo kwa lolote. Kwani hao walikuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara ndiyo yakawafika.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa bila ya shaka tuliwaweka vizuri sio kama tulivyo kuwekeni nyinyi; na tuliwapa masikio, na macho, na nyoyo. Na hayakuwafaa kitu masikio yao, wala macho yao, wala nyoyo zao kwa lolote. Kwani hao walikuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na yale waliyo kuwa wakiyafanyia maskhara ndiyo yakawazunguka.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70