وَيَوْمَ يُعْرَضُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ عَلَى ٱلنَّارِ أَذْهَبْتُمْ طَيِّبَٰتِكُمْ فِى حَيَاتِكُمُ ٱلدُّنْيَا وَٱسْتَمْتَعْتُم بِهَا فَٱلْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ ٱلْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ فِى ٱلْأَرْضِ بِغَيْرِ ٱلْحَقِّ وَبِمَا كُنتُمْ تَفْسُقُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku watakapoletwa wale waliokufuru kwenye Moto, wataambiwa: 'Nyinyi mlitwaa vitu vyenu vizuri katika uhai wa duniani, na mkajistarehesha navyo. Basi leo ndio mnalipwa adhabu ya fedheha kwa yale mlivyokuwa mkitakabari katika ardhi bila ya haki, na kwa sababu mlikuwa mkivuka mipaka.'
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa siku watakapo letwa walio kufuru kwenye Moto wataambiwa: Nyinyi mlitwaa vitu vyenu vizuri katika uhai wa duniani, na mkastareheshwa navyo. Basi leo ndio mnalipwa adhabu ya fedheha kwa mlivyo kuwa mkitakabari katika ardhi bila ya haki, na kwa sababu mlikuwa mkifanya upotovu.