Mwanzo › Sura › Sura Al-Bayyina
Sura Al-Bayyina البينة
Aya 8 · Madina · mpangilio wa kuteremshwa 100
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ لَمْ يَكُنِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْ أَهْلِ ٱلْكِتَٰبِ وَٱلْمُشْرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ ٱلْبَيِّنَةُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hawakuwa waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache waliyo nayo mpaka iwajie bayana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
رَسُولٌ مِّنَ ٱللَّهِ يَتْلُوا۟ صُحُفًا مُّطَهَّرَةً
Swahili Translation - Rowad Translation Center Yaani Mtume aliyetoka kwa Mwenyezi Mungu anayewasomea kurasa zilizotakasika.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فِيهَا كُتُبٌ قَيِّمَةٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ndani yake mna maandiko yaliyonyooka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا تَفَرَّقَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَٰبَ إِلَّا مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَتْهُمُ ٱلْبَيِّنَةُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala hawakufarikiana waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia hiyo bayana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَآ أُمِرُوٓا۟ إِلَّا لِيَعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ حُنَفَآءَ وَيُقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤْتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ وَذَٰلِكَ دِينُ ٱلْقَيِّمَةِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْ أَهْلِ ٱلْكِتَٰبِ وَٱلْمُشْرِكِينَ فِى نَارِ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أُو۟لَٰٓئِكَ هُمْ شَرُّ ٱلْبَرِيَّةِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo. Hao ndio viumbe waovu kabisa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ أُو۟لَٰٓئِكَ هُمْ خَيْرُ ٱلْبَرِيَّةِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika walioamini na wakatenda mema, hao ndio bora wa viumbe.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
جَزَآؤُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّٰتُ عَدْنٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا رَّضِىَ ٱللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا۟ عَنْهُ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِىَ رَبَّهُۥ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Malipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za mbinguni za daima, zipitazo mito kati yake. Wakae humo milele. Mwenyezi Mungu yu radhi nao, na wao wa radhi naye. Hayo ni kwa anayemwogopa Mola wake Mlezi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Al-Qadr
Sura Az-Zalzala →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.