caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Saba سبإ

Aya 54 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 58

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى لَهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ وَلَهُ ٱلْحَمْدُ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ وَهُوَ ٱلْحَكِيمُ ٱلْخَبِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye ni vyake vyote vilivyo mbinguni na katika ardhi. Na sifa ni zake Yeye katika Akhera. Naye ni Mwenye hekima, Mwenye habari.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِى ٱلْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا وَهُوَ ٱلرَّحِيمُ ٱلْغَفُورُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda huko. Na Yeye ni Mwenye kurehemu, Mwenye kusamehe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَا تَأْتِينَا ٱلسَّاعَةُ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّى لَتَأْتِيَنَّكُمْ عَٰلِمِ ٱلْغَيْبِ لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِى ٱلْأَرْضِ وَلَآ أَصْغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكْبَرُ إِلَّا فِى كِتَٰبٍ مُّبِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walisema wale waliokufuru: "Haitatufikia Saa ya Kiyama." Sema: Kwani, hapana shaka itakufikieni, ninaapa kwa haki ya Mola wangu Mlezi, Mwenye kujua ya ghaibu! Hapana kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi, isipokuwa vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenye kubainisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِّيَجْزِىَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ أُو۟لَٰٓئِكَ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli awalipe wale walioamini na wakatenda mema. Hao watapata msamaha na riziki ya ukarimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ سَعَوْ فِىٓ ءَايَٰتِنَا مُعَٰجِزِينَ أُو۟لَٰٓئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مِّن رِّجْزٍ أَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliojitahidi kuzipinga Ishara zetu wakaona watashinda, hao watapata adhabu mbaya yenye uchungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَرَى ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ ٱلَّذِىٓ أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ هُوَ ٱلْحَقَّ وَيَهْدِىٓ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلْعَزِيزِ ٱلْحَمِيدِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliopewa elimu wanaona ya kuwa yale uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ndiyo haki, nayo huongoa kwendea njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ هَلْ نَدُلُّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ يُنَبِّئُكُمْ إِذَا مُزِّقْتُمْ كُلَّ مُمَزَّقٍ إِنَّكُمْ لَفِى خَلْقٍ جَدِيدٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliokufuru walisema: Je, tuwajulisheni mtu anayewaambieni kwamba mtakapochambuliwa mapande mapande mtakuwa katika umbo jipya?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَم بِهِۦ جِنَّةٌۢ بَلِ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ فِى ٱلْعَذَابِ وَٱلضَّلَٰلِ ٱلْبَعِيدِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAma amemzulia Mwenyezi Mungu uongo, au ana wazimu. Bali wale wasioamini Akhera wamo adhabuni na upotovu wa mbali kabisa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَلَمْ يَرَوْا۟ إِلَىٰ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ إِن نَّشَأْ نَخْسِفْ بِهِمُ ٱلْأَرْضَ أَوْ نُسْقِطْ عَلَيْهِمْ كِسَفًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّكُلِّ عَبْدٍ مُّنِيبٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani hawaoni yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, ya mbingu na ardhi? Tungelipenda, tungeliwadidimiza ndani ya ardhi, au tungeliwateremshia juu yao vipande vya mbingu. Hakika katika haya zipo Ishara kwa kila mja aliyetubia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا دَاوُۥدَ مِنَّا فَضْلًا يَٰجِبَالُ أَوِّبِى مَعَهُۥ وَٱلطَّيْرَ وَأَلَنَّا لَهُ ٱلْحَدِيدَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tulimpa Daudi fadhila kutoka kwetu, tukasema: "Enyi milima, karirini kumtakasa Mwenyezi Mungu pamoja naye! Na ndege pia." Na tukamlainishia chuma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَنِ ٱعْمَلْ سَٰبِغَٰتٍ وَقَدِّرْ فِى ٱلسَّرْدِ وَٱعْمَلُوا۟ صَٰلِحًا إِنِّى بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTukamwambia: "Tengeneza nguo za chuma pana, na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika Mimi nayaona vyema mnayoyatenda."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلِسُلَيْمَٰنَ ٱلرِّيحَ غُدُوُّهَا شَهْرٌ وَرَوَاحُهَا شَهْرٌ وَأَسَلْنَا لَهُۥ عَيْنَ ٱلْقِطْرِ وَمِنَ ٱلْجِنِّ مَن يَعْمَلُ بَيْنَ يَدَيْهِ بِإِذْنِ رَبِّهِۦ وَمَن يَزِغْ مِنْهُمْ عَنْ أَمْرِنَا نُذِقْهُ مِنْ عَذَابِ ٱلسَّعِيرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye Suleiman tuliufanya upepo umtumikie. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamyeyushia chemichemi ya shaba. Na katika majini, walikuwako waliokuwa wakifanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na kila anayejitenga na amri yetu katika wao, tunamuonjesha adhabu ya Moto unaowaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَعْمَلُونَ لَهُۥ مَا يَشَآءُ مِن مَّحَٰرِيبَ وَتَمَٰثِيلَ وَجِفَانٍ كَٱلْجَوَابِ وَقُدُورٍ رَّاسِيَٰتٍ ٱعْمَلُوٓا۟ ءَالَ دَاوُۥدَ شُكْرًا وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِىَ ٱلشَّكُورُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na vitu vifananavyo vingine, na madeste makubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yaliyo madhubuti. Enyi watu wa Daudi, fanyeni kazi kwa kushukuru. Na ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّا قَضَيْنَا عَلَيْهِ ٱلْمَوْتَ مَا دَلَّهُمْ عَلَىٰ مَوْتِهِۦٓ إِلَّا دَآبَّةُ ٱلْأَرْضِ تَأْكُلُ مِنسَأَتَهُۥ فَلَمَّا خَرَّ تَبَيَّنَتِ ٱلْجِنُّ أَن لَّوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ ٱلْغَيْبَ مَا لَبِثُوا۟ فِى ٱلْعَذَابِ ٱلْمُهِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tulipomhukumia kufa, hapana aliyewajulisha kufa kwake ila mnyama wa ardhi aliyekula fimbo yake. Na alipoanguka, majini wakatambua lau kuwa wangelijua ya ghaibu wasingelikaa katika adhabu hiyo ya kufedhehesha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَقَدْ كَانَ لِسَبَإٍ فِى مَسْكَنِهِمْ ءَايَةٌ جَنَّتَانِ عَن يَمِينٍ وَشِمَالٍ كُلُوا۟ مِن رِّزْقِ رَبِّكُمْ وَٱشْكُرُوا۟ لَهُۥ بَلْدَةٌ طَيِّبَةٌ وَرَبٌّ غَفُورٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika ilikuwepo Ishara kwa (watu wa nchi ya) Sabaa katika maskani yao - bustani mbili, kulia na kushoto. Kuleni katika riziki ya Mwenyezi Mungu, na mumshukuru. Mji mzuri na Mola Mlezi aliye Msamehevu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَعْرَضُوا۟ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ سَيْلَ ٱلْعَرِمِ وَبَدَّلْنَٰهُم بِجَنَّتَيْهِمْ جَنَّتَيْنِ ذَوَاتَىْ أُكُلٍ خَمْطٍ وَأَثْلٍ وَشَىْءٍ مِّن سِدْرٍ قَلِيلٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini wakayapa mgongo. Kwa hivyo, tukawatumia mafuriko makubwa, na tukawabadilishia badala ya bustani zao hizo kwa bustani nyingine zenye matunda makali, machungu, na mivinje, na kidogo katika miti ya kunazi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ جَزَيْنَٰهُم بِمَا كَفَرُوا۟ وَهَلْ نُجَٰزِىٓ إِلَّا ٱلْكَفُورَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo tuliwalipa kwa sababu ya walivyokufuru. Nasi kwani tunamuadhibu isipokuwa anayekufuru?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ ٱلْقُرَى ٱلَّتِى بَٰرَكْنَا فِيهَا قُرًى ظَٰهِرَةً وَقَدَّرْنَا فِيهَا ٱلسَّيْرَ سِيرُوا۟ فِيهَا لَيَالِىَ وَأَيَّامًا ءَامِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa baina yao na miji mingine tuliyoibariki tuliweka miji iliyo dhahiri, na tukaweka humo vituo vya safari. Tukawaambia, "Nendeni humo usiku na mchana kwa amani."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَقَالُوا۟ رَبَّنَا بَٰعِدْ بَيْنَ أَسْفَارِنَا وَظَلَمُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ فَجَعَلْنَٰهُمْ أَحَادِيثَ وَمَزَّقْنَٰهُمْ كُلَّ مُمَزَّقٍ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَٰتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini wakasema, "Mola wetu Mlezi! Weka mwendo mrefu baina ya safari zetu." Na wakazidhulumu nafsi zao. Basi tukawafanya ni masimulizi tu, na tukawatawanya tawanya. Hakika katika hayo bila ya shaka zimo Ishara kwa kila mwenye kusubiri sana na akashukuru mno.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ صَدَّقَ عَلَيْهِمْ إِبْلِيسُ ظَنَّهُۥ فَٱتَّبَعُوهُ إِلَّا فَرِيقًا مِّنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka Iblisi aliihakikisha ile dhana yake juu yao. Nao walimfuata, isipokuwa kundi katika Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا كَانَ لَهُۥ عَلَيْهِم مِّن سُلْطَٰنٍ إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يُؤْمِنُ بِٱلْـَٔاخِرَةِ مِمَّنْ هُوَ مِنْهَا فِى شَكٍّ وَرَبُّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ حَفِيظٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa yeye hakuwa na mamlaka yoyote juu yao, isipokuwa kwa sababu ya kuwajaribu ili tumjue ni nani mwenye kuamini Akhera, na ni nani anayeitilia shaka. Na Mola wako Mlezi ni Mwenye kuhifadhi kila kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلِ ٱدْعُوا۟ ٱلَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِى ٱلْأَرْضِ وَمَا لَهُمْ فِيهِمَا مِن شِرْكٍ وَمَا لَهُۥ مِنْهُم مِّن ظَهِيرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema, "Waiteni wale mnaowadaia kuwa ni badala ya Mwenyezi Mungu. Hawamiliki hata uzito wa chembe katika mbingu wala ardhi. Wala hawana ushirika wowote humo. Wala Yeye hana msaidizi miongoni mwao."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تَنفَعُ ٱلشَّفَٰعَةُ عِندَهُۥٓ إِلَّا لِمَنْ أَذِنَ لَهُۥ حَتَّىٰٓ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا۟ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ قَالُوا۟ ٱلْحَقَّ وَهُوَ ٱلْعَلِىُّ ٱلْكَبِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala uombezi mbele yake hautafaa kitu, isipokuwa kwa aliyempa idhini. Hata itakapoondolewa hofu kwenye nyoyo zao, watasema: "Mola wenu Mlezi amesema nini?" Watasema: "Yaliyo kweli! Na Yeye ndiye Aliye juu, Mkubwa."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ قُلِ ٱللَّهُ وَإِنَّآ أَوْ إِيَّاكُمْ لَعَلَىٰ هُدًى أَوْ فِى ضَلَٰلٍ مُّبِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu! Na hakika sisi au nyinyi bila ya shaka tuko kwenye uongofu au upotovu ulio wazi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُل لَّا تُسْـَٔلُونَ عَمَّآ أَجْرَمْنَا وَلَا نُسْـَٔلُ عَمَّا تَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Nyinyi hamtaulizwa makosa tuliyoyafanya, wala sisi hatutaulizwa mnayoyatenda nyinyi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ يَجْمَعُ بَيْنَنَا رَبُّنَا ثُمَّ يَفْتَحُ بَيْنَنَا بِٱلْحَقِّ وَهُوَ ٱلْفَتَّاحُ ٱلْعَلِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mola wetu Mlezi atatukusanya, kisha atatuhukumu kwa haki; na Yeye ndiye Hakimu, Mwenye kujua vyema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ أَرُونِىَ ٱلَّذِينَ أَلْحَقْتُم بِهِۦ شُرَكَآءَ كَلَّا بَلْ هُوَ ٱللَّهُ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Nionyesheni mliowaunganisha naye kuwa washirika. Hasha! Bali Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَرْسَلْنَٰكَ إِلَّا كَآفَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَٰدِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanasema: "Ahadi hii itakuwa lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli?"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُل لَّكُم مِّيعَادُ يَوْمٍ لَّا تَسْتَـْٔخِرُونَ عَنْهُ سَاعَةً وَلَا تَسْتَقْدِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: "Nyinyi mnayo miadi ya Siku ambayo hamtakawiya mbali nayo kwa saa moja, wala hamtaitangulia."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَن نُّؤْمِنَ بِهَٰذَا ٱلْقُرْءَانِ وَلَا بِٱلَّذِى بَيْنَ يَدَيْهِ وَلَوْ تَرَىٰٓ إِذِ ٱلظَّٰلِمُونَ مَوْقُوفُونَ عِندَ رَبِّهِمْ يَرْجِعُ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ ٱلْقَوْلَ يَقُولُ ٱلَّذِينَ ٱسْتُضْعِفُوا۟ لِلَّذِينَ ٱسْتَكْبَرُوا۟ لَوْلَآ أَنتُمْ لَكُنَّا مُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walisema wale waliokufuru, "Hatutaiamini Qur-ani hii, wala yale yaliyokuwa kabla yake." Na ungeliwaona madhalimu watakaposimamishwa mbele ya Mola wao Mlezi, wakirudishiana maneno wao kwa wao! Wanyonge wakiwaambia wale waliotakabari, "Lau kuwa si nyinyi, bila ya shaka tungelikuwa Waumini sisi."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ ٱلَّذِينَ ٱسْتَكْبَرُوا۟ لِلَّذِينَ ٱسْتُضْعِفُوٓا۟ أَنَحْنُ صَدَدْنَٰكُمْ عَنِ ٱلْهُدَىٰ بَعْدَ إِذْ جَآءَكُم بَلْ كُنتُم مُّجْرِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliotakabari watawaambia wanyonge, "Kwani sisi ndio tuliwazuia na uongofu baada ya huo kukujieni? Bali nyinyi wenyewe ni wahalifu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ ٱلَّذِينَ ٱسْتُضْعِفُوا۟ لِلَّذِينَ ٱسْتَكْبَرُوا۟ بَلْ مَكْرُ ٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ إِذْ تَأْمُرُونَنَآ أَن نَّكْفُرَ بِٱللَّهِ وَنَجْعَلَ لَهُۥٓ أَندَادًا وَأَسَرُّوا۟ ٱلنَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُا۟ ٱلْعَذَابَ وَجَعَلْنَا ٱلْأَغْلَٰلَ فِىٓ أَعْنَاقِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ هَلْ يُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanyonge wakawaambia wale waliotakabari, "Bali ni vitimbi vyenu vya usiku na mchana, mlipokuwa mkituamrisha tumkufuru Mwenyezi Mungu, na tumfanyie washirika." Nao wataficha majuto watakapoiona adhabu. Na tutaweka makongwa shingoni mwa wale waliokufuru. Kwani wanalipwa isipokuwa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَرْسَلْنَا فِى قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَآ إِنَّا بِمَآ أُرْسِلْتُم بِهِۦ كَٰفِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hatukumtuma mwonyaji yeyote kwenye mji, isipokuwa walisema wale waliojidekeza kwa starehe zao, wa mji huo, "Hakika sisi tunayakataa hayo mliyotumwa nayo."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالُوا۟ نَحْنُ أَكْثَرُ أَمْوَٰلًا وَأَوْلَٰدًا وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakasema, "Sisi tuna mali nyingi zaidi na watoto, wala sisi hatutaadhibiwa."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ إِنَّ رَبِّى يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقْدِرُ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema, "Hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye. Lakini watu wengi hawajui."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَمْوَٰلُكُمْ وَلَآ أَوْلَٰدُكُم بِٱلَّتِى تُقَرِّبُكُمْ عِندَنَا زُلْفَىٰٓ إِلَّا مَنْ ءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحًا فَأُو۟لَٰٓئِكَ لَهُمْ جَزَآءُ ٱلضِّعْفِ بِمَا عَمِلُوا۟ وَهُمْ فِى ٱلْغُرُفَٰتِ ءَامِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa si mali zenu wala watoto wenu watakaowasongesha karibu na sisi, muwe karibu sana, isipokuwa yule aliyeamini na akatenda mema. Hao basi watapata malipo maradufu kwa yale waliyoyafanya. Nao watakuwa salama katika maghorofa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ يَسْعَوْنَ فِىٓ ءَايَٰتِنَا مُعَٰجِزِينَ أُو۟لَٰٓئِكَ فِى ٱلْعَذَابِ مُحْضَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale wanaojitahidi kuzipinga Ishara zetu, wakaona watashinda, hao watahudhurishwa kwenye adhabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ إِنَّ رَبِّى يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ وَيَقْدِرُ لَهُۥ وَمَآ أَنفَقْتُم مِّن شَىْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُۥ وَهُوَ خَيْرُ ٱلرَّٰزِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: "Kwa hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye katika waja wake. Na chochote mtakachokitoa, Yeye atakilipa. Naye ni Mbora wa wanaoruzuku."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ يَقُولُ لِلْمَلَٰٓئِكَةِ أَهَٰٓؤُلَآءِ إِيَّاكُمْ كَانُوا۟ يَعْبُدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku atakayowakusanya wote, kisha atawaambia Malaika, "Je, hawa walikuwa wakikuabuduni?"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ سُبْحَٰنَكَ أَنتَ وَلِيُّنَا مِن دُونِهِم بَلْ كَانُوا۟ يَعْبُدُونَ ٱلْجِنَّ أَكْثَرُهُم بِهِم مُّؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaseme, "Subhanak (umetakasika). Wewe ndiye kipenzi chetu, si hao. Bali wao walikuwa wakiwaabudu majini; wengi wao wakiwaamini hao."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱلْيَوْمَ لَا يَمْلِكُ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ نَّفْعًا وَلَا ضَرًّا وَنَقُولُ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ ذُوقُوا۟ عَذَابَ ٱلنَّارِ ٱلَّتِى كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi hii leo hataweza yeyote kumletea nafuu wala madhara mwenziwe. Na tutawaambia wale waliodhulumu, "Onjeni adhabu ya Moto mliokuwa mkiukadhibisha."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ءَايَٰتُنَا بَيِّنَٰتٍ قَالُوا۟ مَا هَٰذَآ إِلَّا رَجُلٌ يُرِيدُ أَن يَصُدَّكُمْ عَمَّا كَانَ يَعْبُدُ ءَابَآؤُكُمْ وَقَالُوا۟ مَا هَٰذَآ إِلَّآ إِفْكٌ مُّفْتَرًى وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِلْحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمْ إِنْ هَٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wanasema: "Huyu si chochote isipokuwa ni mtu anayetaka kuwazuia na yale waliyokuwa wakiabudu baba zenu." Na wakasema: "Haya si chochote isipokuwa ni uongo uliozuliwa." Na wale waliokufuru waliiambia haki ilipowajia: "Haya si chochote isipokuwa ni uchawi ulio dhahiri."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ ءَاتَيْنَٰهُم مِّن كُتُبٍ يَدْرُسُونَهَا وَمَآ أَرْسَلْنَآ إِلَيْهِمْ قَبْلَكَ مِن نَّذِيرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala hatukuwapa Vitabu wavisome, wala hatukuwatumia mwonyaji kabla yako wewe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَمَا بَلَغُوا۟ مِعْشَارَ مَآ ءَاتَيْنَٰهُمْ فَكَذَّبُوا۟ رُسُلِى فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walikadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Na hawakufikia hata sehemu moja katika kumi ya tulivyowapa hao. Nao waliwakadhibisha Mitume wangu. Basi kuangamiza kwangu kulikuwa namna gani!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ إِنَّمَآ أَعِظُكُم بِوَٰحِدَةٍ أَن تَقُومُوا۟ لِلَّهِ مَثْنَىٰ وَفُرَٰدَىٰ ثُمَّ تَتَفَكَّرُوا۟ مَا بِصَاحِبِكُم مِّن جِنَّةٍ إِنْ هُوَ إِلَّا نَذِيرٌ لَّكُم بَيْنَ يَدَىْ عَذَابٍ شَدِيدٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: "Mimi ninawanasihi kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili wawili na mmoja mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu huyu hana wazimu. Yeye si chochote isipokuwa ni mwonyaji kwenu kabla ya kufika adhabu kali."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ مَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ فَهُوَ لَكُمْ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: "Ujira niliowaomba ni wenu nyinyi. Sina ujira isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ni Shahidi juu ya kila kitu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ إِنَّ رَبِّى يَقْذِفُ بِٱلْحَقِّ عَلَّٰمُ ٱلْغُيُوبِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: "Hakika Mola wangu Mlezi anaondoa upotovu kwa haki. Yeye ndiye Mwenye kujua vyema ya ghaibu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ جَآءَ ٱلْحَقُّ وَمَا يُبْدِئُ ٱلْبَٰطِلُ وَمَا يُعِيدُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: "Kweli imefika, na batili haijitokezi, wala hairudi."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ إِن ضَلَلْتُ فَإِنَّمَآ أَضِلُّ عَلَىٰ نَفْسِى وَإِنِ ٱهْتَدَيْتُ فَبِمَا يُوحِىٓ إِلَىَّ رَبِّىٓ إِنَّهُۥ سَمِيعٌ قَرِيبٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: "Ikiwa mimi nimepotea, basi nimepotea kwa kudhuru nafsi yangu mwenyewe. Na ikiwa nimeongoka, basi ni kwa sababu ya kunifunulia Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, aliye karibu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْ تَرَىٰٓ إِذْ فَزِعُوا۟ فَلَا فَوْتَ وَأُخِذُوا۟ مِن مَّكَانٍ قَرِيبٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau ungeliona watakapobabaika, basi hapana pa kukimbilia! Na watakamatwa mahala pa karibu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالُوٓا۟ ءَامَنَّا بِهِۦ وَأَنَّىٰ لَهُمُ ٱلتَّنَاوُشُ مِن مَّكَانٍۭ بَعِيدٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watasema: "Tunaiamini!" Lakini wataipata wapi kutoka huko mahali mbali?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَدْ كَفَرُوا۟ بِهِۦ مِن قَبْلُ وَيَقْذِفُونَ بِٱلْغَيْبِ مِن مَّكَانٍۭ بَعِيدٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hapo kabla yake waliikataa, na wakiyatupilia mbali maneno ya ghaibu kutoka mahali mbali.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَحِيلَ بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ مَا يَشْتَهُونَ كَمَا فُعِلَ بِأَشْيَاعِهِم مِّن قَبْلُ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ فِى شَكٍّ مُّرِيبٍۭ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watatiliwa kizuizi baina yao na hayo wanayoyatamani, kama walivyofanyiwa wenzao zamani. Hakika hao walikuwa na shaka ya kutia wasiwasi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70