أَفَلَمْ يَرَوْا۟ إِلَىٰ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ إِن نَّشَأْ نَخْسِفْ بِهِمُ ٱلْأَرْضَ أَوْ نُسْقِطْ عَلَيْهِمْ كِسَفًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّكُلِّ عَبْدٍ مُّنِيبٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani hawaoni yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, ya mbingu na ardhi? Tungelipenda, tungeliwadidimiza ndani ya ardhi, au tungeliwateremshia juu yao vipande vya mbingu. Hakika katika haya zipo Ishara kwa kila mja aliyetubia.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniKwani hawaoni yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao ya mbingu na ardhi? Tungeli penda tungeli wadidimiza ndani ya ardhi, au tungeli wateremshia juu yao vipande vya mbingu. Hakika katika haya zipo Ishara kwa kila mja aliye tubia.