caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Fath, Aya 15

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 111 · 48:15

سَيَقُولُ ٱلْمُخَلَّفُونَ إِذَا ٱنطَلَقْتُمْ إِلَىٰ مَغَانِمَ لِتَأْخُذُوهَا ذَرُونَا نَتَّبِعْكُمْ يُرِيدُونَ أَن يُبَدِّلُوا۟ كَلَٰمَ ٱللَّهِ قُل لَّن تَتَّبِعُونَا كَذَٰلِكُمْ قَالَ ٱللَّهُ مِن قَبْلُ فَسَيَقُولُونَ بَلْ تَحْسُدُونَنَا بَلْ كَانُوا۟ لَا يَفْقَهُونَ إِلَّا قَلِيلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale waliobaki nyuma watasema: 'Mtakapokwenda kuchukua ngawira, tuacheni tukufuateni!' Wanataka kuyabadili maneno ya Mwenyezi Mungu. Sema: 'Hamtatufuata kabisa. Mwenyezi Mungu alikwisha sema hivi zamani.' Hapo watasema: 'Bali nyinyi mnatuhusudu.' Sivyo, bali walikuwa hawafahamu ila kidogo.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWalio baki nyuma watasema: Mtapo kwenda kuchukua ngawira, tuacheni tukufuateni! Wanataka kuyabadili maneno ya Mwenyezi Mungu. Sema: Hamtatufuata kabisa. Mwenyezi Mungu alikwisha sema kama hivi zamani. Hapo watasema: Bali nyinyi mnatuhusudu. Siyo, bali walikuwa hawafahamu ila kidogo.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70