قُل لِّلْمُخَلَّفِينَ مِنَ ٱلْأَعْرَابِ سَتُدْعَوْنَ إِلَىٰ قَوْمٍ أُو۟لِى بَأْسٍ شَدِيدٍ تُقَٰتِلُونَهُمْ أَوْ يُسْلِمُونَ فَإِن تُطِيعُوا۟ يُؤْتِكُمُ ٱللَّهُ أَجْرًا حَسَنًا وَإِن تَتَوَلَّوْا۟ كَمَا تَوَلَّيْتُم مِّن قَبْلُ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaambie wale walioachwa nyuma katika mabedui: 'Mtakuja itwa kwenda kupigana na watu wakali kwa vita, mpigane nao au wasalimu amri. Basi mkimtii, Mwenyezi Mungu atawapa ujira mzuri. Na mkigeuka kama mlivyogeuka kwanza, atawaadhibu kwa adhabu iliyo chungu.'
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWaambie walio achwa nyuma katika mabedui: Mtakuja itwa kwenda pigana na watu wakali kwa vita, mpigane nao au wasalimu amri. Basi mkimt'ii, Mwenyezi Mungu atakupeni ujira mzuri. Na mkigeuka kama mlivyo geuka kwanza, atakuadhibuni kwa adhabu iliyo chungu.