caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Fath, Aya 11

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 111 · 48:11

سَيَقُولُ لَكَ ٱلْمُخَلَّفُونَ مِنَ ٱلْأَعْرَابِ شَغَلَتْنَآ أَمْوَٰلُنَا وَأَهْلُونَا فَٱسْتَغْفِرْ لَنَا يَقُولُونَ بِأَلْسِنَتِهِم مَّا لَيْسَ فِى قُلُوبِهِمْ قُلْ فَمَن يَمْلِكُ لَكُم مِّنَ ٱللَّهِ شَيْـًٔا إِنْ أَرَادَ بِكُمْ ضَرًّا أَوْ أَرَادَ بِكُمْ نَفْعًۢا بَلْ كَانَ ٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًۢا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatakuambia mabedui waliobaki nyuma: 'Zimetushughulisha mali zetu na ahali zetu, basi tuombee msamaha.' Wanasema kwa ndimi zao yasiyokuwamo katika nyoyo zao. Sema: 'Ni nani awezaye kukusaidieni chochote kwa Mwenyezi Mungu akitaka Yeye kuwadhuru au akitaka kuwanufaisha? Bali Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.'
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWatakuambia mabedui walio baki nyuma: Yametushughulisha mali yetu na ahali zetu, basi tuombee msamaha. Wanasema kwa ndimi zao yasiyo kuwamo katika nyoyo zao. Sema: Ni nani awezaye kukusaidieni chochote kwa Mwenyezi Mungu akitaka Yeye kukudhuruni au akitaka kukunufaisheni? Bali Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70