وَعَدَكُمُ ٱللَّهُ مَغَانِمَ كَثِيرَةً تَأْخُذُونَهَا فَعَجَّلَ لَكُمْ هَٰذِهِۦ وَكَفَّ أَيْدِىَ ٱلنَّاسِ عَنكُمْ وَلِتَكُونَ ءَايَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ وَيَهْدِيَكُمْ صِرَٰطًا مُّسْتَقِيمًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu anawaahidi ngawira nyingi mtakazozichukua, basi amewatangulizia hizi kwanza, na akaizuia mikono ya watu isiwafikie, na ili hayo yawe ni Ishara kwa Waumini, na akawaongoza njia iliyonyooka.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu anakuahidini ngawira nyingi mtakazo zichukua, basi amekutangulizieni hizi kwanza, na akaizuia mikono ya watu isikufikieni, na ili hayo yawe ni Ishara kwa Waumini, na akakuongozeni Njia Iliyo Nyooka.