caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Fath, Aya 17

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 111 · 48:17

لَّيْسَ عَلَى ٱلْأَعْمَىٰ حَرَجٌ وَلَا عَلَى ٱلْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَى ٱلْمَرِيضِ حَرَجٌ وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ يُدْخِلْهُ جَنَّٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَٰرُ وَمَن يَتَوَلَّ يُعَذِّبْهُ عَذَابًا أَلِيمًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKipofu hana lawama, wala kiguru hana lawama, wala mgonjwa hana lawama. Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, atamuingiza katika Mabustani ya mbinguni yapitayo mito chini yake. Na atakayegeuka upande, atamuadhibu kwa adhabu chungu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniKipofu hana lawama, wala kiguru hana lawama, wala mgonjwa hana lawama. Na mwenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, atamuingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Na atakaye geuka upande atamuadhibu kwa adhabu chungu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70