Swahili Translation - Rowad Translation CenterVinamtakasa Mwenyezi Mungu vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Musa alipowaambia watu wake: 'Enyi watu wangu! Kwa nini mnaniudhi, nanyi mnajua kuwa hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu niliyetumwa kwenu?' Walipokengeuka, Mwenyezi Mungu akazipotoa nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wavukao mipaka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Isa mwana wa Mariamu aliposema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakayekuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipowaletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhahiri!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo, naye anaitwa kwenye Uislamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na Dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote, ijapokuwa washirikina watachukia.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMuaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na piganeni Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu. Haya ni bora kwenu, ikiwa nyinyi mnajua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAtakusameheni dhambi zenu, na atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake, na maskani mazuri mazuri katika Bustani za milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu, kama alivyosema Isa mwana Mariamu kuwaambia wanafunzi wake: 'Ni nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu?' Wakasema wanafunzi: 'Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu!' Basi kundi moja la Wana wa Israili liliamini, na kundi jingine lilikufuru. Basi tukawaunga mkono wale walioamini dhidi ya maadui zao, wakawa wenye kushinda.