Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mwenyezi Mungu amekwishasikia usemi wa mwanamke anayejadiliana nawe juu ya mumewe, na anamlalamikia Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anayasikia majibizano yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia mno, Mwenye kuona zaidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale miongoni mwenu wanaowasawazisha wake zao na mama zao, hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale waliowazaa. Na hakika hao wanasema neno ovu mno, na la uongo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi mno, Mwenye kusamehe zaidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale wanaojitenga na wake zao, kisha wakarudia katika yale waliyoyasema, basi wamkomboe mtumwa kabla hawajagusana. Mnapewa maonyo kwa hayo. Na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayoyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa asiyepata mtumwa kumkomboa, basi na afunge saumu miezi miwili mfululizo kabla hawajagusana. Na asiyeweza hayo, basi awalishe masikini sitini. Hayo ni hivyo ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na makafiri watapata adhabu chungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wanaopinzana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, watadhalilishwa kama walivyodhalilishwa wale waliokuwa kabla yao. Na tulikwishateremsha Ishara zilizo wazi. Na makafiri watapata adhabu ya kufedhehesha.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku atakapowafufua Mwenyezi Mungu, na awaambie yale waliyoyatenda. Mwenyezi Mungu ameyadhibiti, na wao wameyasahau! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu anajua vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi? Hauwi mnong'ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wanne wao, wala wa watano ila Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache kuliko hao, wala walio wengi zaidi, ila Yeye yu pamoja nao popote pale walipo. Kisha Siku ya Kiyama atawaambia waliyoyatenda. Hakika Mwenyezi Mungu anajua zaidi kila kitu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani huwaoni wale waliokatazwa kunong'onezana, kisha wakayarudia yale yale waliyokatazwa, na wakanong'ona juu ya mambo ya dhambi, na ya uadui, na ya kumuasi Mtume? Na wakikujia, hukuamkua sivyo anavyokuamkua Mwenyezi Mungu. Na husema katika nafsi zao: 'Mbona Mwenyezi Mungu hatuadhibu kwa haya tuyasemayo?' Basi Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Na hayo ndiyo marejeo maovu yaliyoje!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Mnaponong'ona, msinong'one kwa sababu ya mambo ya madhambi, na uadui, na kumuasi Mtume. Bali nong'onezeni kwa kutenda mema na kuacha maovu. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye kwake mtakusanywa nyote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika minong'ono hiyo inatokana na Shetani ili awahuzunishe wale walioamini, na wala haitawadhuru chochote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na juu ya Mwenyezi Mungu tu ndio wategemee Waumini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Mkiambiwa: Fanyeni nafasi katika mabaraza, basi fanyeni nafasi. Na Mwenyezi Mungu atakufanyieni nyinyi nafasi. Na mkiambiwa: "Ondokeni", basi ondokeni. Mwenyezi Mungu atawainua wale walioamini miongoni mwenu, na wale waliopewa elimu daraja za juu. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kusemezana kwenu. Hiyo ni heri kwenu na usafi zaidi. Na ikiwa hamkupata cha kutoa, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe mno, Mwenye kurehemu zaidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMnachelea kutanguliza hiyo sadaka kabla ya kusemezana kwenu kwa siri? Ikiwa hamkufanya hayo, na Mwenyezi Mungu akapokea toba yenu, basi simamisheni Sala, na toeni Zaka, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuwaoni wale waliofanya urafiki mwendani na watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia? Hao si katika nyinyi, wala si katika wao. Na huapa kwa uongo hali ya kuwa wanajua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWamefanya viapo vyao ni ngao, na wakaizuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi hao watapata adhabu ya kufedhehesha.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayatawafaa kitu mali yao wala watoto wao mbele ya Mwenyezi Mungu. Hao ndio watu wa Motoni. Humo watadumu milele.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku atakayowafufua Mwenyezi Mungu wote, wamuapie kama wanavyokuapieni nyinyi. Na watadhani kuwa wamepata kitu! Kwa hakika hao ndio waongo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterShetani amewatawala na akawasahaulisha kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hao ndio kundi la Shetani. Sikilizeni, hakika kundi la Shetani ndilo lenye kuhasirika.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu ameandika: Hapana shaka Mimi na Mtume wangu tutashinda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuwakuti watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa daima. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio Hizbullahi (Kundi la Mwenyezi Mungu). Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa.