مِّنَ ٱلَّذِينَ هَادُوا۟ يُحَرِّفُونَ ٱلْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِۦ وَيَقُولُونَ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَٱسْمَعْ غَيْرَ مُسْمَعٍ وَرَٰعِنَا لَيًّۢا بِأَلْسِنَتِهِمْ وَطَعْنًا فِى ٱلدِّينِ وَلَوْ أَنَّهُمْ قَالُوا۟ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا وَٱسْمَعْ وَٱنظُرْنَا لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَقْوَمَ وَلَٰكِن لَّعَنَهُمُ ٱللَّهُ بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMiongoni mwa Mayahudi wamo wanaopotosha maneno kuyatoa pahali pake, na husema: 'Tumesikia na tumeasi, na sikia bila ya kusikizishwa.' Na husema: "Raai'naa", kwa kuzipotoa ndimi zao na kuitukana Dini. Na lau kama wangelisema: "Tumesikia na tumetii, na usikie na "Undhurna (utuangalie)," ingelikuwa heri kwao na ya unyoofu zaidi. Lakini Mwenyezi Mungu aliwalaani kwa kufuru yao; basi hawaamini isipokuwa wachache tu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniMiongoni mwa Mayahudi wamo ambao hubadilisha maneno kuyatoa mahala pake, na husema: Tumesikia na tumeasi, na sikia bila ya kusikilizwa. Na husema: "Raai'naa", kwa kuzipotoa ndimi zao ili kuitukana Dini. Na lau kama wangeli sema: Tumesikia na tumet'ii, na usikie na "Undhurna" (Utuangalie), ingeli kuwa ni kheri kwao na sawa zaidi. Lakini Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru yao; basi hawaamini ila wachache tu.