وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُم بِهِۦ مِنْ خِطْبَةِ ٱلنِّسَآءِ أَوْ أَكْنَنتُمْ فِىٓ أَنفُسِكُمْ عَلِمَ ٱللَّهُ أَنَّكُمْ سَتَذْكُرُونَهُنَّ وَلَٰكِن لَّا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّآ أَن تَقُولُوا۟ قَوْلًا مَّعْرُوفًا وَلَا تَعْزِمُوا۟ عُقْدَةَ ٱلنِّكَاحِ حَتَّىٰ يَبْلُغَ ٱلْكِتَٰبُ أَجَلَهُۥ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِىٓ أَنفُسِكُمْ فَٱحْذَرُوهُ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala hakuna ubaya juu yenu katika kupeleka posa kwa ishara tu kwa wanawake walio katika eda au mkalificha ndani ya nyoyo zenu. Mwenyezi Mungu alikwishajua kwamba nyinyi mtawakumbuka. Lakini msiwaahidi kwa siri, isipokuwa mseme maneno mema. Wala msiazimie kufunga mkataba wa ndoa mpaka andiko (la amri ya eda) lifike muda wake. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu kwa hakika anajua yaliyo katika nafsi zenu. Basi jitahadharini naye. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mpole.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWala si vibaya kwenu katika kupeleka posa kwa ishara tu kwa wanawake waliomo edani au mkadhamiria katika nyoyo zenu. Mwenyezi Mungu anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka. Lakini msiwaahidi kwa siri, ila mnene maneno mema. Wala msiazimie kufunga ndoa mpaka eda ifike mwisho wake. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo katika nafsi zenu. Basi tahadharini naye. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mpole.