caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 234

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:234

وَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَٰجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا فَعَلْنَ فِىٓ أَنفُسِهِنَّ بِٱلْمَعْرُوفِ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale miongoni mwenu wanaofishwa, na wanaacha wake, hawa wake wazizuie nafsi zao miezi minne na siku kumi. Na wanapotimiza muda wao (wa eda), basi hakuna ubaya wowote juu yao katika yale wanayojifanyia kwa wema. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wale miongoni mwenu wanao kufa na wakaacha wake, hawa wake wangoje peke yao miezi mine na siku kumi. Na wanapo timiza eda yao basi hapana ubaya kwao kwa wanao jifanyia kwa mujibu wa ada. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70