Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanapokujia wanafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni Mtume wake, na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanafiki ni waongo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWamevifanya viapo vyao ni ngao, na wao wakaizuia Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika ni mabaya kabisa waliyokuwa wakiyafanya.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru; kwa hivyo zikazibwa nyoyo zao. Kwa hivyo hawafahamu lolote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa unapowaona, miili yao inakupendeza, na wakisema, unasikiliza usemi wao. Lakini wao ni kama magogo yaliyoegemezwa. Wao hudhania kila ukelele unaopigwa ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; tahadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka mbali na haki?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSawa sawa kwao, ukiwatakia maghfira au hukuwatakia maghfira, Mwenyezi Mungu hatawaghufiria. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wavukao mipaka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ndio wanaosema: Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, ili waondokelee mbali! Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye hazina za mbingu na ardhi, lakini wanafiki hawafahamu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanasema: Tukirejea Madina, mwenye utukufu zaidi bila ya shaka atamfukuza humo aliye mnyonge. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu, na Mtume wake, na Waumini. Lakini wanafiki hawajui.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Zisikusahaulisheni mali zenu, wala watoto wenu, kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na wenye kufanya hayo, basi hao ndio waliohasiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa toeni katika tulichokupeni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, tena hapo akasema: 'Mola wangu Mlezi! Huniakhirishi muda kidogo, nipate kutoa sadaka sana, na niwe katika watu wema?'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala Mwenyezi Mungu hataiakhirisha nafsi yoyote unapofika muda wake. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.