فَهَزَمُوهُم بِإِذْنِ ٱللَّهِ وَقَتَلَ دَاوُۥدُ جَالُوتَ وَءَاتَىٰهُ ٱللَّهُ ٱلْمُلْكَ وَٱلْحِكْمَةَ وَعَلَّمَهُۥ مِمَّا يَشَآءُ وَلَوْلَا دَفْعُ ٱللَّهِ ٱلنَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّفَسَدَتِ ٱلْأَرْضُ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ ذُو فَضْلٍ عَلَى ٱلْعَٰلَمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hivyo, wakawashinda kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na Daudi akamuua Jaluti. Na Mwenyezi Mungu akampa Daudi ufalme na hekima, na akamfundisha katika aliyoyataka. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawazuii watu kwa watu, basi dunia ingeliharibika. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya walimwengu wote.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani--Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu waliwatimua, na Daudi akamuuwa Jaluti, na Mwenyezi Mungu akampa Daudi ufalme na hikima, na akamfundisha aliyo yapenda. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawapambanishi watu kwa watu basi dunia ingeli haribika. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya walimwengu wote.