يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ ٱللَّهُ يُفْتِيكُمْ فِى ٱلْكَلَٰلَةِ إِنِ ٱمْرُؤٌا۟ هَلَكَ لَيْسَ لَهُۥ وَلَدٌ وَلَهُۥٓ أُخْتٌ فَلَهَا نِصْفُ مَا تَرَكَ وَهُوَ يَرِثُهَآ إِن لَّمْ يَكُن لَّهَا وَلَدٌ فَإِن كَانَتَا ٱثْنَتَيْنِ فَلَهُمَا ٱلثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَ وَإِن كَانُوٓا۟ إِخْوَةً رِّجَالًا وَنِسَآءً فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ ٱلْأُنثَيَيْنِ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمْ أَن تَضِلُّوا۟ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌۢ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanakuuliza hukumu ya kisheria, sema: Mwenyezi Mungu anawapa hukumu ya kisheria juu ya kalala (mtu aliyekufa bila ya kuacha mzazi wala mwana). Ikiwa mtu amekufa, naye hana mwana, lakini anaye dada, basi huyo atapata nusu ya alichokiacha. Naye (mwanamume) atamrithi (dada yake) ikiwa hana mwana. Na ikiwa wao ni madada wawili, basi watapata theluthi mbili za alichokiacha. Na wakiwa ndugu wanaume na wanawake, basi wa kiume atapata sehemu iliyo sawa na ya wa kike wawili. Mwenyezi Mungu anawabainishia ili msipotee. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWanakuomba uhukumu, sema: Mwenyezi Mungu anakupeni hukumu juu ya mkiwa. Ikiwa mtu amekufa, naye hana mtoto, lakini anaye ndugu wa kike, basi huyo atapata nusu alicho acha maiti. Na mwanamume atamrithi ndugu wa kike ikiwa hana mwana. Na ikiwa wao ni ndugu wa kike wawili, basi watapata thuluthi mbili za alicho acha maiti. Na wakiwa ndugu wanaume na wanawake, basi mwanamume atapata sehemu iliyo sawa na ya wanawake wawili. Mwenyezi Mungu anakubainishieni ili msipotee; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.