caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 286

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:286

لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا ٱكْتَسَبَتْ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَآ إِن نَّسِينَآ أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَآ إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِنَا رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِۦ وَٱعْفُ عَنَّا وَٱغْفِرْ لَنَا وَٱرْحَمْنَآ أَنتَ مَوْلَىٰنَا فَٱنصُرْنَا عَلَى ٱلْقَوْمِ ٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kiwango cha iwezavyo. Faida ya iliyoyachuma ni yake, na hasara ya iliyoyachuma ni juu yake pia. (Semeni) Mola wetu Mlezi! Usituchukulie ubaya tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama uliyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi! Usitutwike tusiyoyaweza, na uyatupilie mbali mabaya yetu, na utusamehe na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi dhidi ya kaumu ya makafiri.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyho. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia. (Ombeni:)Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70