لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَىٰهُمْ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَهْدِى مَن يَشَآءُ وَمَا تُنفِقُوا۟ مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ٱبْتِغَآءَ وَجْهِ ٱللَّهِ وَمَا تُنفِقُوا۟ مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSi juu yako wewe kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na chochote mnachotoa katika heri, basi ni cha nafsi zenu. Wala hamtoi isipokuwa kwa kutafuta uso wa Mwenyezi Mungu. Na chochote mnachotoa katika heri, mtalipwa kwa ukamilifu, nanyi hamtadhulumiwa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniSi juu yako wewe kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na kheri yoyote mnayo toa ni kwa nafsi zenu. Wala msitoe ila kwa kutafuta wajihi wa Mwenyezi Mungu. Na kheri yoyote mtakayo toa mtalipwa kwa ukamilifu, wala hamtadhulumiwa.