caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 259

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:259

أَوْ كَٱلَّذِى مَرَّ عَلَىٰ قَرْيَةٍ وَهِىَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا قَالَ أَنَّىٰ يُحْىِۦ هَٰذِهِ ٱللَّهُ بَعْدَ مَوْتِهَا فَأَمَاتَهُ ٱللَّهُ مِا۟ئَةَ عَامٍ ثُمَّ بَعَثَهُۥ قَالَ كَمْ لَبِثْتَ قَالَ لَبِثْتُ يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ قَالَ بَل لَّبِثْتَ مِا۟ئَةَ عَامٍ فَٱنظُرْ إِلَىٰ طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمْ يَتَسَنَّهْ وَٱنظُرْ إِلَىٰ حِمَارِكَ وَلِنَجْعَلَكَ ءَايَةً لِّلنَّاسِ وَٱنظُرْ إِلَى ٱلْعِظَامِ كَيْفَ نُنشِزُهَا ثُمَّ نَكْسُوهَا لَحْمًا فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُۥ قَالَ أَعْلَمُ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu kama yule aliyepita karibu na mji hali ya kuwa umekwishakuwa magofu tu. Akasema: Vipi Mwenyezi Mungu ataufufua mji huu baada ya kufa kwake? Basi Mwenyezi Mungu akamfisha yeye (muda wa) miaka mia moja, kisha akamfufua. Akasema: Je umekaa muda gani? Akasema: (Labda) nimekaa siku moja au sehemu ya siku. Akasema: Bali umekaa miaka mia moja. Hebu angalia chakula chako na vinywaji vyako, havikuharibika. Na mwangalie punda wako. Na ili tukufanye uwe ni ishara kwa watu. Na iangalie mifupa yake hii jinsi tunavyoinyanyua kisha tuivishe nyama. Basi yalipombainikia, alisema: Ninajua kwamba kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo mno juu ya kila kitu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniAu kama yule aliye pita karibu na mji ulio kwisha kuwa magofu tu, akasema: Ataufufuaje Mwenyezi Mungu mji huu baada ya kufa kwake? Basi Mwenyezi Mungu alimfisha yeye muda wa miaka mia. Kisha akamfufua. Akamuuliza: Je umekaa muda gani? Akajibu: Labda nimekaa siku moja au sehemu ya siku. Akamwambia: Bali umekaa miaka mia wewe. Hebu angalia chakula chako na vinywaji vyako, havikuharibika. Na muangalie punda wako. Na ili tukufanye uwe ni Ishara kwa watu iangalie hii mifupa yake jinsi tunavyo inyanyua kisha tunaivisha nyama. Basi yalipo mbainikia alinena: Najua kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70