caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nisaa, Aya 77

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 92 · 4:77

أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ قِيلَ لَهُمْ كُفُّوٓا۟ أَيْدِيَكُمْ وَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ ٱلْقِتَالُ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَخْشَوْنَ ٱلنَّاسَ كَخَشْيَةِ ٱللَّهِ أَوْ أَشَدَّ خَشْيَةً وَقَالُوا۟ رَبَّنَا لِمَ كَتَبْتَ عَلَيْنَا ٱلْقِتَالَ لَوْلَآ أَخَّرْتَنَآ إِلَىٰٓ أَجَلٍ قَرِيبٍ قُلْ مَتَٰعُ ٱلدُّنْيَا قَلِيلٌ وَٱلْـَٔاخِرَةُ خَيْرٌ لِّمَنِ ٱتَّقَىٰ وَلَا تُظْلَمُونَ فَتِيلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hukuwaona wale walioambiwa: ‘Izuieni mikono yenu, na mshike Swala na mtoe Zaka.’ Na pindi walipoamrishwa kupigana, mara kundi moja miongoni mwao likawaogopa watu kama kumwogopa Mwenyezi Mungu, au kwa hofu kubwa zaidi. Na wakasema: ‘Mola wetu Mlezi! Kwa nini umetuamrisha kupigana? Laiti ungetuahirishia kiasi ya muda kidogo hivi!’ Sema: ‘Starehe ya dunia ni ndogo, na Akhera ni bora zaidi kwa mwenye kucha Mungu. Wala hamtadhulumiwa hata kijiuzi kilicho ndani ya uwazi wa kokwa ya tende.’
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniJe, huwaoni wale walio ambiwa: Izuieni mikono yenu, na mshike Swala na mtoe Zaka. Na walipo amrishwa kupigana, mara kundi moja kati yao liliwaogopa watu kama kumwogopa Mwenyezi Mungu, au kwa khofu kubwa zaidi. Na wakasema: Mola Mlezi wetu! Kwa nini umetuamrisha kupigana? Laiti unge tuakhirishia kiasi ya muda kidogo hivi! Sema: Starehe ya dunia ni ndogo, na Akhera ni bora zaidi kwa mwenye kuchamngu. Wala hamtadhulumiwa hata uzi wa kokwa ya tende.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70