يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَقْرَبُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنتُمْ سُكَٰرَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا۟ مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِى سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا۟ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰٓ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَآءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ ٱلْغَآئِطِ أَوْ لَٰمَسْتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَلَمْ تَجِدُوا۟ مَآءً فَتَيَمَّمُوا۟ صَعِيدًا طَيِّبًا فَٱمْسَحُوا۟ بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Msiikaribie Swala hali ya kuwa mmelewa, mpaka myajue mnayoyasema. Wala mkiwa na janaba (msikaribie swala wala msikiti), isipokuwa wanaopita njia (msikitini), mpaka muoge. Na mkiwa wagonjwa, au katika safari, au mmoja wenu akitoka chooni, au mkiwagusa (yaani kuwajamii) wanawake, na msipate maji, basi ukusudieni mchanga safi. Basi upangusieni kwenye nyuso zenu na mikono yenu. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye kufuta dhambi.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniEnyi mlio amini! Msikaribie Sala, hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema, wala hali mna janaba - isipo kuwa mmo safarini - mpaka mkoge. Na mkiwa wagonjwa, au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni, au mmewagusa wanawake - na msipate maji, basi ukusudieni mchanga safi, mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kughufiria.