وَيَسْتَفْتُونَكَ فِى ٱلنِّسَآءِ قُلِ ٱللَّهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِى ٱلْكِتَٰبِ فِى يَتَٰمَى ٱلنِّسَآءِ ٱلَّٰتِى لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَٱلْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ ٱلْوِلْدَٰنِ وَأَن تَقُومُوا۟ لِلْيَتَٰمَىٰ بِٱلْقِسْطِ وَمَا تَفْعَلُوا۟ مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِهِۦ عَلِيمًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanakuuliza fatwa kuhusiana na wanawake. Sema: Mwenyezi Mungu anawatolea fatwa juu yao, na yale mnayosomewa katika Kitabu hiki kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi kile walichoandikiwa, na mnapenda kwamba muwaoe, na kuhusu wanyonge katika watoto, na kwamba muwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na chochote mnachofanya katika heri, basi hakika Mwenyezi Mungu anaijua vyema.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWanakuuliza nini sharia ya wanawake. Sema: Mwenyezi Mungu ana kutoleeni fatwa juu yao, na mnayo somewa humu Kitabuni kukhusu mayatima wanawake ambao hamwapi walicho andikiwa, na mnapenda kuwaoa, na kukhusu wanyonge katika watoto, na kwamba mwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na kheri yoyote mnayo fanya Mwenyezi Mungu anaijua.