caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 267

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:267

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَنفِقُوا۟ مِن طَيِّبَٰتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّآ أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ ٱلْأَرْضِ وَلَا تَيَمَّمُوا۟ ٱلْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِـَٔاخِذِيهِ إِلَّآ أَن تُغْمِضُوا۟ فِيهِ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ غَنِىٌّ حَمِيدٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Toeni katika vile vizuri mlivyovichuma, na katika vile tulivyowatolea katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, ilhali nyinyi wenyewe msingevipokea isipokuwa kwa kuvifumbia macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniEnyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70