caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Baqara, Aya 253

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 87 · 2:253

تِلْكَ ٱلرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ ٱللَّهُ وَرَفَعَ بَعْضَهُمْ دَرَجَٰتٍ وَءَاتَيْنَا عِيسَى ٱبْنَ مَرْيَمَ ٱلْبَيِّنَٰتِ وَأَيَّدْنَٰهُ بِرُوحِ ٱلْقُدُسِ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَا ٱقْتَتَلَ ٱلَّذِينَ مِنۢ بَعْدِهِم مِّنۢ بَعْدِ مَا جَآءَتْهُمُ ٱلْبَيِّنَٰتُ وَلَٰكِنِ ٱخْتَلَفُوا۟ فَمِنْهُم مَّنْ ءَامَنَ وَمِنْهُم مَّن كَفَرَ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَا ٱقْتَتَلُوا۟ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMitume hao tumewaboresha baadhi yao juu ya wengineo. Miongoni mwao kuna wale ambao Mwenyezi Mungu alisema nao, na akawapandisha vyeo baadhi yao. Na tukampa Isa mwana wa Maryam hoja zilizo wazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Mtakatifu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelipenda, wasingelipigana wale waliokuwa baada yao, baada ya kujiwa na hoja zilizo wazi. Lakini walihitilafiana. Basi miongoni mwao kuna wale walioamini, na miongoni mwao kuna wale waliokufuru. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka, wasingelipigana. Lakini Mwenyezi Mungu hufanya kile akitakacho.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniMITUME hao tumewatukuza baadhi yao juu ya wengineo. Katika wao wapo ambao Mwenyezi Mungu alisema nao, na wengine akawapandisha vyeo. Na tukampa Isa mwana wa Mariyam hoja zilizo wazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana walio kuwa baada yao baada ya kuwajia hoja zilizo wazi. Lakini walikhitalifiana. Basi wapo kati yao walio amini, na wengine kati yao walio kufuru. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu alipenda wasingeli pigana. Lakini Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70