لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَبْتَغُوا۟ فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ فَإِذَآ أَفَضْتُم مِّنْ عَرَفَٰتٍ فَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ عِندَ ٱلْمَشْعَرِ ٱلْحَرَامِ وَٱذْكُرُوهُ كَمَا هَدَىٰكُمْ وَإِن كُنتُم مِّن قَبْلِهِۦ لَمِنَ ٱلضَّآلِّينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakuna ubaya wowote juu yenu kutafuta fadhila kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi mtakapomiminika kutoka 'Arafat, mtajeni Mwenyezi Mungu katika Mash'aril Haram (eneo takatifu). Na mtajeni kama alivyowaongoa, ijapokuwa kabla ya hilo mlikuwa miongoni mwa waliopotea.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniSi vibaya kwenu kuitafuta fadhila ya Mola wenu Mlezi. Na mtakapo miminika kutoka A'rafat mtajeni Mwenyezi Mungu penye Masha'ril Haram. Na mkumbukeni kama alivyo kuongoeni, ijapo kuwa zamani mlikuwa miongoni mwa walio potea.