قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِى ٱلسَّمَآءِ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَىٰهَا فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا۟ وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُۥ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَٰبَ لَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa yakini, tuliona unavyougeuzageuza uso wako mbinguni. Basi, tutakuelekeza kwenye Kibla unachokiridhia. Basi, elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu. Na popote mnapokuwa, zielekezeni nyuso zenu upande wake. Na hakika, wale waliopewa Kitabu wanajua sana kwamba hiyo ndiyo haki itokayo kwa Mola wao Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika mbali na yale wanayoyatenda.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniKwa yakini tukiona unavyo geuza geuza uso wako mbinguni. Basi tutakuelekeza kwenye Kibla ukipendacho. Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu; na popote mnapokuwa zielekezeni nyuso zenu upande huo; na hakika wale walio pewa Kitabu wanajua kwamba hiyo ni haki itokayo kwa Mola wao Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale wanayo yatenda.