caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Maaida, Aya 32

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 112 · 5:32

مِنْ أَجْلِ ذَٰلِكَ كَتَبْنَا عَلَىٰ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ أَنَّهُۥ مَن قَتَلَ نَفْسًۢا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِى ٱلْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ ٱلنَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَآ أَحْيَا ٱلنَّاسَ جَمِيعًا وَلَقَدْ جَآءَتْهُمْ رُسُلُنَا بِٱلْبَيِّنَٰتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم بَعْدَ ذَٰلِكَ فِى ٱلْأَرْضِ لَمُسْرِفُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa sababu ya hayo, tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba mwenye kuiua nafsi bila ya nafsi hiyo kuiua nyingine, au kufanya uharibifu katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kuiweka hai, basi ni kama amewaweka hai watu wote. Na hakika walikwishawajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha hakika wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniKwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70