caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nisaa, Aya 94

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 92 · 4:94

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا ضَرَبْتُمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَتَبَيَّنُوا۟ وَلَا تَقُولُوا۟ لِمَنْ أَلْقَىٰٓ إِلَيْكُمُ ٱلسَّلَٰمَ لَسْتَ مُؤْمِنًا تَبْتَغُونَ عَرَضَ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا فَعِندَ ٱللَّهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٌ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبْلُ فَمَنَّ ٱللَّهُ عَلَيْكُمْ فَتَبَيَّنُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Mnaposafiri katika Njia ya Mwenyezi Mungu, basi chunguzeni sawasawa, wala msimwambie anayewatolea salamu: 'Wewe si Muumini'; kwa kutaka manufaa ya maisha ya dunia hii, hali ya kuwa kwa Mwenyezi Mungu ndiko zipo ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa nyinyi zamani, na Mwenyezi Mungu akawaneemesha. Basi chunguzeni sawasawa. Hakika, Mwenyezi Mungu kwa yale mnayoyatenda anazo habari zote.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniEnyi mlio amini! Mnapo safiri katika Njia ya Mwenyezi Mungu basi hakikisheni, wala msimwambie anaye kutoleeni salamu: Wewe si Muumini; kwa kutaka manufaa ya maisha ya dunia hii, hali ya kuwa kwa Mwenyezi Mungu zipo ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyo kuwa nyinyi zamani, na Mwenyezi Mungu akakuneemesheni. Basi chunguzeni sawa sawa. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70