caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nisaa, Aya 90

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 92 · 4:90

إِلَّا ٱلَّذِينَ يَصِلُونَ إِلَىٰ قَوْمٍۭ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَٰقٌ أَوْ جَآءُوكُمْ حَصِرَتْ صُدُورُهُمْ أَن يُقَٰتِلُوكُمْ أَوْ يُقَٰتِلُوا۟ قَوْمَهُمْ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَسَلَّطَهُمْ عَلَيْكُمْ فَلَقَٰتَلُوكُمْ فَإِنِ ٱعْتَزَلُوكُمْ فَلَمْ يُقَٰتِلُوكُمْ وَأَلْقَوْا۟ إِلَيْكُمُ ٱلسَّلَمَ فَمَا جَعَلَ ٱللَّهُ لَكُمْ عَلَيْهِمْ سَبِيلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa wale waliofungamana na kaumu ambao kuna ahadi baina yenu na wao, au wanawajia hali ya kuwa vifua vyao vina dhiki juu ya kupigana nanyi, au kupigana na kaumu yao. Na lau angelipenda Mwenyezi Mungu, angeliwapa mamlaka juu yenu na wangelipigana nanyi. Kwa hivyo, wakijitenga nanyi, na wasipigane nanyi, na wakawaletea amani, basi Mwenyezi Mungu hakuwapa nyinyi njia dhidi yao.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniIsipokuwa wale walio fungamana na watu ambao mna ahadi baina yenu na wao, au wanakujieni na vifua vyao vina dhiki kupigana nanyi, au kupigana na watu wao. Na lau angeli penda Mwenyezi Mungu angeli wasaliti juu yenu wakapigana nanyi. Basi wakijitenga nanyi, wasipigane nanyi, na wakakuleteeni amani, basi Mwenyezi Mungu hakukupeni njia kupigana nao.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70