caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nisaa, Aya 34

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 92 · 4:34

ٱلرِّجَالُ قَوَّٰمُونَ عَلَى ٱلنِّسَآءِ بِمَا فَضَّلَ ٱللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَآ أَنفَقُوا۟ مِنْ أَمْوَٰلِهِمْ فَٱلصَّٰلِحَٰتُ قَٰنِتَٰتٌ حَٰفِظَٰتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ ٱللَّهُ وَٱلَّٰتِى تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَٱهْجُرُوهُنَّ فِى ٱلْمَضَاجِعِ وَٱضْرِبُوهُنَّ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا۟ عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanaume ni wasimamizi imara wa wanawake, kwa yale aliyowafadhilisha kwayo Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa yale wanayoyatoa katika mali zao. Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na wanaojilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na wale mnaochelea kutoka kwao katika utiifu, waaidhini, na wahameni katika malazi, na wapigeni. Basi wakiwatii, msitafute njia yoyote dhidi yao. Hakika, Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu, Mkubwa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70