caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nisaa, Aya 35

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 92 · 4:35

وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَٱبْعَثُوا۟ حَكَمًا مِّنْ أَهْلِهِۦ وَحَكَمًا مِّنْ أَهْلِهَآ إِن يُرِيدَآ إِصْلَٰحًا يُوَفِّقِ ٱللَّهُ بَيْنَهُمَآ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mkihofia kuwepo mfarakano baina ya wawili hao, basi mtumeni mpatanishi kutoka kwa jamaa za mume, na mpatanishi kutoka kwa jamaa za mke. Ikiwa wanataka kutengeneza mambo, Mwenyezi Mungu ataleta maafikiano kati yao. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye habari zote.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70