وَلِكُلٍّ جَعَلْنَا مَوَٰلِىَ مِمَّا تَرَكَ ٱلْوَٰلِدَانِ وَٱلْأَقْرَبُونَ وَٱلَّذِينَ عَقَدَتْ أَيْمَٰنُكُمْ فَـَٔاتُوهُمْ نَصِيبَهُمْ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kila mmoja tumemfanyia warithi katika yale waliyoyaacha wazazi wawili na jamaa. Na wale mliofungamana nao kwa viapo, wapeni fungu lao. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Shahidi juu ya kila kitu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa kila mmoja tumemwekea warithi katika waliyo yaacha wazazi wawili na jamaa. Na mlio fungamana nao ahadi wapeni fungu lao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa kila kitu.