وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا ٱلْمَسِيحَ عِيسَى ٱبْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ ٱللَّهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ ٱخْتَلَفُوا۟ فِيهِ لَفِى شَكٍّ مِّنْهُ مَا لَهُم بِهِۦ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا ٱتِّبَاعَ ٱلظَّنِّ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًۢا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kusema kwao: 'Hakika, sisi tulimuua Masihi Isa, mwana wa Maryam, Mtume wa Mwenyezi Mungu.' Nao hawakumuua wala hawakumsulubisha, bali walifananishiwa tu. Na hakika wale waliohitilafiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana elimu yoyote nayo isipokuwa ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuua kwa yakini.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini.