caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nisaa, Aya 153

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 92 · 4:153

يَسْـَٔلُكَ أَهْلُ ٱلْكِتَٰبِ أَن تُنَزِّلَ عَلَيْهِمْ كِتَٰبًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فَقَدْ سَأَلُوا۟ مُوسَىٰٓ أَكْبَرَ مِن ذَٰلِكَ فَقَالُوٓا۟ أَرِنَا ٱللَّهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْهُمُ ٱلصَّٰعِقَةُ بِظُلْمِهِمْ ثُمَّ ٱتَّخَذُوا۟ ٱلْعِجْلَ مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَتْهُمُ ٱلْبَيِّنَٰتُ فَعَفَوْنَا عَن ذَٰلِكَ وَءَاتَيْنَا مُوسَىٰ سُلْطَٰنًا مُّبِينًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatu wa Kitabu wanakuuliza uwateremshie kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika, walikwishamuuliza Musa makubwa zaidi ya hayo. Walisema: 'Tuonyeshe Mwenyezi Mungu wazi wazi.' Kwa hivyo, radi ikawapiga kwa dhuluma yao hiyo. Kisha wakamchukua ndama kumwabudu, baada ya kwishawajia hoja zilizo wazi. Nasi tukasamehe hayo, na tukampa Musa hoja zilizo dhahiri.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWatu wa Kitabu wanakutaka uwateremshia kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika walikwisha mtaka Musa makubwa kuliko hayo. Walisema: Tuonyeshe Mwenyezi Mungu wazi wazi. Wakapigwa na radi kwa hiyo dhulma yao. Kisha wakamchukua ndama kumuabudu, baada ya kwisha wajia hoja zilizo wazi. Nasi tukasamehe hayo, na tukampa Musa nguvu zilizo dhaahiri.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70