caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nisaa, Aya 113

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 92 · 4:113

وَلَوْلَا فَضْلُ ٱللَّهِ عَلَيْكَ وَرَحْمَتُهُۥ لَهَمَّت طَّآئِفَةٌ مِّنْهُمْ أَن يُضِلُّوكَ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمْ وَمَا يَضُرُّونَكَ مِن شَىْءٍ وَأَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَيْكَ ٱلْكِتَٰبَ وَٱلْحِكْمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمْ تَكُن تَعْلَمُ وَكَانَ فَضْلُ ٱللَّهِ عَلَيْكَ عَظِيمًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako na rehema yake, kundi moja kati yao lingedhamiria kukupoteza. Na hawapotezi isipokuwa nafsi zao, wala hawawezi kukudhuru kwa lolote. Na Mwenyezi Mungu amekuteremshia Kitabu na hekima, na akakufundisha yale uliyokuwa huyajui. Na fadhila za Mwenyezi Mungu zilizo juu yako ni kubwa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako na rehema yake, kundi moja kati yao linge dhamiria kukupoteza. Wala hawapotezi ila nafsi zao, wala hawawezi kukudhuru kwa lolote. Na Mwenyezi Mungu amekuteremshia Kitabu na hikima na amekufundisha uliyo kuwa huyajui. Na fadhila za Mwenyezi Mungu zilizo juu yako ni kubwa.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70